London , England
MANCHESTER United jana ilionyesha kuwa
imefufuka kutoka usingizini baada ya
kuichapa Aston Villa mabao 3- 0 kwenye
mchezo mkali wa Ligi Kuu ya England .
Ushindi huu ulikuwa muhimu kwa United
ambayo msimu huu imekuwa na kasi ya
kusuasua na kabla ya mchezo wa jana
ilikuwa ikishika nafasi ya tisa. Sasa
imepanda nafasi moja hadi ya nane.
Katika mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja
wa Villa Park, Danny Welbeck alikuwa shujaa
baada ya kufanikiwa kuifungia timu yake
mabao mawili .
Welbeck aliifungia United bao la kwanza
katika dakika ya 15 baada ya kuuwahi mpira
uliogonga mwamba baada ya kupigwa
kichwa na Januzaj aliyewahi krosi ya Antonio
Valencia.
Welbeck alitupia bao la pili wavuni dakika
tatu baadaye baada ya kuiwahi krosi kutoka
kwa Valencia ambaye alionekana kuwa
mwiba mkali kwenye mchezo huo .
United ilikwenda mapumziko ikiwa mbele kwa
mabao hayo mawili , kipindi cha pili vijana
hao wa Kocha David Moyes walionekana
kuendelea kuja juu na kufanikiwa kufunga
bao la tatu katika dakika ya 52 , kupitia kwa
Tom Cleverley ambaye alipata pasi safi
kutoka kwa Wayne Rooney .
Ushindi huu umewafanya United wafikishe
pointi 25 na kusogea hadi nafasi ya nane
kwenye msimamo huku Aston Villa wakiwa
kwenye nafasi ya 11 na pointi 19.
Mchezo mwingine uliopigwa jana, Norwich
ilifanikiwa kupata sare ya bao 1- 1 ilipovaana
na Swansea kwenye Uwanja wa Carrow
Road.
Nathan Dyer aliifungia Swansea katika dakika
ya 12 huku Gary Hooper, akisawazisha dakika
ya 45 .
Monday, December 16, 2013
United yafufuka , yaifumua Aston Villa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment