Prodyuza chipukizi kwenye tasnia hiyo Bond Bin
Sinnon amechanwa ile mbaya na mshabiki wa
mtangazaji mwenye rekodi ya kuanza fani hiyo
akiwa na umri mdogo “ 13” Lulu Hemagongo
huku wakimtaka Prodyuza huyo kuacha kuongea
kitu mbele ya Aunt Lulu kutokana na msaada
mkubwa alioupata toka mtangazaji huyo hadi leo
hii anaonekana mtu flani kwenye jamii.
Wakiongea na XDEEJAYZ ambayo ndiyo
iliyokuwa ya kwanza kuripo taarifa mahusiano
ya Bond na Wastara kabla ya habari hiyo
kusambaa kwenye mitandao mingine, mashabiki
hao walisema kuwa Bond amekosea sana
kusema kuwa Lulu anatafuta umaarufu kupitia
kwake wakati yeye ndiye aliyepata jina kupitia
Lulu kwani ndiye aliyempatia nafasi ya kupewa
kipindi Channel Ten huku akimuhangaikia mambo
mengi tu hadi leo hii anaonekan Bond.
Mashabiki hao waliongeza kuieleza XDEEJAYZ
na kusema kuwa Bond hakuwa na nyuma wala
mbele lakini Lulu alikuwa msaada mkubwa
kwake ambapo alianza kumtambulisha kwa
wadau hapa mjini pamoja na kumpeleka kwa
mguu wake hadi Channel Ten pamoja kampuni
ya Beknet Production ambako ndiko alikoajiliwa
hadi sasa huko kote huko Lulu ndiye aliyekuwa
akimshika mkono kumuonesha mji unavyoenda.
Aidha nao watu wa karibu na Bond walioneshwa
kushangazwa na kauri ya Bond ya kuwa Lulu
anataka umaarufu kupitia yeye jambo ambalo sio
kweli Bond” Kwanza Lulu alishamuacha Bond
muda mrefu sana zaidi ya miaka miwili sasa
huku kila mmoja anafanya yake sasa haingii
akilini kwamba kwanza Lulu ni msomi kuliko
Bond na hata leo hii Wastara kamuona yeye
kupitia Lulu sasa iweje aseme kuwa Lulu
anamuonea wivu huu ni ukosefu wa fikra”
Alisema Alfan Mohamed ambae ni rafiki wa
karibu.
Hata hivyo Lulu alipotafutwa kupitia simu yake
mkononi alipatikana na kusema kuwa hataki
kuzungumzia chochote kuhusu hilo kwani Mungu
mwenyewe ndiye anaejua
Wednesday, December 4, 2013
BIFU ZITO: MASHABIKI WA AUNT LULU WAMVUA NGUO BOND WA WASTARA, WAMWAMBIA BILA LULU KUMTEMBEZA MJINI HAKUNA MTU ANGEMJUA!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment