Mwandishi wa gazeti la Championi, Khatim
Naheka ( kushoto) , akimkabidhi kocha wa
makipa wa Simba , James Kisaka kiasi cha
Sh 350 ,000 zilizotolewa na gazeti la
Championi pamoja na Mwenyekiti wa kamati
ya usajili ya Simba , Zacharia Hanspope ili
kusaidia matibabu . Kulia ni Mhariri Kiongozi
wa gazeti hilo , Saleh Ally akishuhudia tukio
hilo nyumbani kwa Kisaka .
... Mwandishi wa gazeti la Championi , Khatim
Naheka ( kushoto) , akimpa mkono kocha wa
makipa wa Simba, James Kisaka , Kulia ni
Mhariri Kiongozi wa gazeti la Championi ,
Saleh Ally akishuhudia tukio hilo nyumbani
kwa Kisaka .
Kisaka, kipa wa zamani wa Volcano ya Kenya
amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa
unaosababisha mwili wake kukosa nguvu
upande mmoja ingawa mwenyewe amesema
si kupooza kama ilivyoelezwa awali .
Amekuwa akiendelea na matibabu , hata
hivyo , Kisaka alilalama kushindwa kuhimili
gharama kubwa ya matibabu hivyo
kuwaomba wadau wajitokeze kumsaidia.
Championi likachukua nafasi ya kuomba
wadau wajitokeze kumsaidia lakini uamuzi
ukawa ni kuanza kuwa mfano kwa kutoa
angalau kiasi cha fedha ili kuwahamasisha
wadau kumsaidia Kisaka ambaye hata
kutembea , analazimika kusaidiwa .
Friday, December 6, 2013
CHAMPIONI, HANSPOPE WAMSAIDIA MATIBABU KOCHA SIMBA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Daaaaah hadi raha
ReplyDelete