KUNA mambo mengine ni vigumu kufikiri
kama yanaweza, siyo tu kutamkwa , bali
kutendwa na mtu anayetegemewa na jamii
kama mmoja wa vioo vyake. Kama ambavyo
nimekuwa nikisema siku zote, watu maarufu
wanaotokana na sanaa, wanastahili kuwa
mfano.
Nimesema watu maarufu wanaotokana na
sanaa, maana tunao baadhi ya wenzetu
wana majina makubwa sana na
yanayotamkwa kila mara ndani ya jamii yetu,
lakini wakiwa na sifa zisizofaa . Wengine
wanatambulika kwa ujambazi , uhusiano wa
jinsia moja , utapeli na kadhalika . Hawa siyo
mastaa ninaowalenga!
Mastaa, kwa maana ya wacheza filamu ,
wanasoka , wanamuziki na hata wanasiasa ,
wanapaswa kuwa makini sana kwa kila
jambo wanalolisema na hata kulifanya.
Neno lao lolote , linachukuliwa kwa uzito wa
aina yake mtaani , kwa sababu tu wao ni
watu wa aina yake katika jamii yetu.
Siku kadhaa zilizopita nilikutana na habari ya
huyu binti , mcheza filamu Coletha Raymond .
Katika habari hiyo iliyoandikwa gazetini,
msanii huyo alisema baada ya kutendwa na
mwanaume wake wa zamani , sasa hahitaji
tena kidume kingine , badala yake, anajikita
katika unywaji wa pombe , kwa kile
alichosema , kinampunguzia sana hamu ya
ku - duu!
Coletha, kama nilivyosema, ni staa , msanii
mwenye mashabiki wanaopenda sanaa
anayoifanya. Kitu kimoja amewafundisha
mashabiki wake , hasa watoto , kuwa kumbe
pombe inaweza kumuondolea mtu hamu ya
kupenda kushiriki tendo la ndoa !
Huu ni utani , tena mbaya . Sina uhakika na
utafiti wa kitaalamu kuhusu pombe , lakini
uzoefu unaonyesha watu wengi hujikuta
wakifanya vitendo vya aibu, ikiwemo ngono
zembe , baada ya kufakamia kinywaji.
Maneno haya yana tafsiri nyingi , hasa kama
ni mtu unayefuatilia sana habari za mastaa
wa Kibongo, hasa waigizaji kama Coletha na
wale wa Bongo Fleva . Mojawapo ya ujumbe
ambao mtu anaweza kuupata kwa kusikiliza
kauli hii , ni kwamba msichana huyu hana mtu
na kama atakuwa naye , basi si wa kudumu .
Pombe ni starehe lakini yenye gharama
kubwa , kifedha na kimatokeo . Mtu anaweza
kunywa pombe ya fedha kidogo, lakini
akajikuta akiigharamia kwa kiasi kikubwa cha
pesa kutokana na kile kinachotokana na huo
ulabu aliopiga.
Anaweza akatukana watu , akafanya fujo
zinazoweza kusababisha uharibifu mkubwa
wa mali na vitendo vyake visivyo na
tahadhari kutokana na pombe , vinaweza
kusababisha tukio lolote baya.
Kwa Coletha kuiambia jamii kuwa
anaichukulia pombe kama mbadala wa
wanaume, ni jambo gumu kidogo kulielewa
kwa haraka . Ni kweli , katika unywaji wa
pombe, watu wametofautiana. Wapo ambao
baada ya kupata , hutamani kushiriki tendo la
ndoa ( na hawa ni wengi ) , wengine huwa
wazungumzaji sana na baadhi yao, hugeuka
kuwa wakimya na wenye aibu.
Sijui kundi alilopo huyu mdada , ingawa
uzoefu unaonyesha kuwa mastaa wetu wengi
wanaokunywa pombe hushiriki mambo yetu
yale.
Hata hivyo , kuhamasisha unywaji pombe ,
kama mbadala wa kitu chochote , siyo
ushauri mzuri kutolewa kwa jamii kama yetu,
ambayo imezungukwa na umasikini mkubwa.
Huenda Coletha anao uwezo wa kuhimili
vishindo vya kinywaji, lakini kwa wale
wenzangu na mimi , hili linaweza
kuwaongezea tatizo zaidi badala ya
kuwapunguzia.
Coletha angeweza kunyamaza, lakini kama
alilazimika kusema sababu za kutohitaji
mwanaume baada ya kutendwa , mazoezi
lilikuwa ni jibu zuri zaidi linaloweza kumsaidia
mtu kupunguza hamu ya kushiriki tendo la
ndoa.
Kama ninavyosema mara zote, mastaa wetu
wanao wajibu mkubwa wa kuisaidia jamii
yetu yenye mambo mengi. Kuisaidia siyo
kwenda katika vituo vya watoto yatima na
watu wasiojiweza na kupeleka sabuni na pipi,
bali kupitia kauli na matendo yao.
Friday, December 13, 2013
COLETHA , HUTAKI MWANAUME , UNAPIGA MITUNGI!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kila mtu na ufaham wake wa mambo ye ufaham wake unaishia hapo
ReplyDelete