MSANII wa muziki wa mduara , Zuwena
Mohamed ‘ Shilole ’ amejikuta katika wakati
mgumu baada ya kuandika juu ya uzushi wa
kifo cha msanii mkongwe , Said Ngamba
‘ Mzee Small ’ kupitia mtandao wa
Instargram .
Said Ngamba ‘ Mzee Small ’ aliyezushiwa kifo
Shilole ambaye baada ya kugundua kuwa
hakuwa sahihi kuandika juu ya kifo hicho
kwani haikuwa kweli , alilazimika kukanusha
na ndipo akaanza kuporomoshewa ‘ mvua ’ ya
matusi .
Baadhi ya maneno makali yaliyoandikwa
mtandaoni humo kumtukana Shilole, ambayo
hayawezi kuandikika gazetini kwa kuzingatia
maadili, yalimtaka kujiepusha na tabia ya
kudandia na kueneza mambo pasipo
kuyafanyia uchunguzi.
Zuwena Mohamed ‘Shilole ’.
Mwandishi wetu alipomtafuta msanii huyo
kuzungumzia juu ya suala hilo, alikiri
kuandika juu ya kifo hicho huku akionesha
majuto ya hali ya juu .
“Ni kweli niliandika maneno ya taarifa za kifo
cha Mzee Small , japo nilikuwa nikiandika jinsi
ambavyo msanii huyo amezushiwa kifo, sasa
watu wakadhani mimi ndiye nimeandika kwa
kujitungia , najuta sana kuchapisha ujumbe
huo, ” alisema Shilole.
Friday, December 13, 2013
UZUSHI WA KIFO CHA MZEE SMALL, SHILOLE YAMKUTA!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Ukiwa na dam ya kunguni bana
ReplyDelete