Monday, December 16, 2013

Kaseja : Waleteni hao Simba SC


Kipa mpya wa Yanga , Juma Kaseja .
Na Wilbert Molandi
KIPA mpya wa Yanga, Juma Kaseja,
amesema yupo tayari muda na wakati
wowote kucheza mechi dhidi ya timu yake ya
zamani, Simba.
Kaseja ametoa kauli hiyo juzi Jumamosi
mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa
kirafiki dhidi ya KMKM ya Zanzibar kwa ajili
ya kujiandaa na mechi ya Mtani Jembe
itakayowakutanisha Simba na Yanga kwenye
Uwanja wa Taifa , Dar es Salaam, Jumamosi
ijayo .
Akizungumza na Championi Jumatatu, Kaseja
alisema ana uzoefu mkubwa wa kucheza
mechi kati ya timu hizo mbili .
Kaseja alisema mechi hiyo haihofii na yupo
fiti kwa ajili ya kukabiliana na Simba
kutokana na maandalizi anayoyafanya chini
ya kocha wake Mkenya , Razack Siwa.
“Nina uzoefu mkubwa wa kucheza mechi hizi
ngumu za Simba na Yanga mara
zinapokutana, hivyo sihofii kabisa , nipo tayari
kucheza muda wowote .
“Kwa bahati nzuri nimewahi kuzichezea timu
hizo zote kwa wakati tofauti , hivyo nazijua
vizuri, kikubwa ninaendelea na maandalizi ya
nguvu kuhakikisha ninafanya vizuri, ” alisema
Kaseja.

No comments:

Post a Comment

.