Wednesday, December 4, 2013

DAH HII NI NOMA SANA...!! SERENGETI BOY AJIUA BAADA YA KUTOSWA NA SHUGA MUMI WA KI NIGERIA...!!


Kijana mmoja kutoka Nigeria aliyefahamika kwa
jina la Michael Jaja(22) ameamua kujirestisha In
Peace baada ya mwanamke aliyekuwa akimlea
wanaofahamika kwa jina la shuga mami(48)
kumtaka wavunje uhusiano wao kutokana na ujio
wa ghafla wa mume wake ambaye alikuwa
akiishi nje ya nchi kwa miaka kadhaa.
Katika Picha ni Michael Jaja na Mwanamke
aliyekuwa akimpa jeuri (Shuga mami) wakila
bata Dubai.
Chanzo kimoja cha habari kutoka Nigeria
kilieleza kwamba Jaja alikuwa ameshazoea
maisha ya raha na starehe aliyokuwa akipewa na
mama kubwa huyo mpaka kufikia hatua ya
kununuliwa gari ya kutembelea aina ya Toyota
Corolla kama zawadi sambamba na safari za
kwenda Dubai na China kula bata vilevile kuishi
katika jumba la kifahari la mwanamke huyo
aliyekuwa akimpa jeuri mjini.
Baada ya mwanamke huyo kumwambia
waachane kutokana na ujio wa mume wake
huyo, Jaja alitishia kumuua na kujiua kama
ataachwa kutokana na kufikiria kurudia katika
hali yake ya msoto kama zamani, habari
zinasema kwamba walipokea taarifa za mtu
kujiua kwa kitu kinachodhaniwa ni bastola na
ndipo ripoti za polisi zilipobainisha kuwa
aliyekufa alikuwa ni Michael jaja na hata baada
ya mwanamke yule alipoenda kutoa salamu za
pole kwa mama aliyetambulishwa kuwa ndiye
mkwe wake aliambiwa kwamba alidanganywa na
kijana huyo, hii sio mara ya kwanza kwa vijana
wa Nigeria kuamua kujiua kutokana na mikasa
kama huu uliomtokea Jaja.

No comments:

Post a Comment

.