Thursday, December 12, 2013

DUDE AKIRI USHIRIKINA KUUA SANAA!


MSANII wa filamu za Kibongo, Kulwa
Kikumba ‘ Dude ’ ameibuka na kusema
sababu ya tasnia ya filamu kudorora na sasa
inaelekea kufa kabisa ni kutokana na
ushirikina wa wasanii .
Kulwa Kikumba ‘Dude ’ .
‘ Akistorisha’ na gazeti hili , Dude alisema
wasanii wa filamu wamekuwa wakiendekeza
sana ushirikina , kitu ambacho kinasababisha
tasnia hiyo kudorora kwani wengi
wanapoteza muda kwa waganga wa kienyeji
kwa madai kuwa wanaenda kupandisha
nyota wawe mastaa na baada ya hapo
wanaanza kuringa .
“Utakuta msanii anafanya vizuri sana
mwanzo anapoingia kwenye tasnia lakini
baada ya muda anaanza kufifia akiona hivyo
anakimbilia kwa mganga matokeo yake
anajibweteka .”

No comments:

Post a Comment

.