Thursday, December 12, 2013

KOLETA ATOBOA SIRI YA KUCHUKIA WANAUME!


Na Brighton Masalu
MSANII wa maigizo na filamu , Coletha
Raymond ‘ Koleta’ amefunguka na kutoboa
siri ya moyoni juu ya chanzo cha kuwachukia
wanaume huku akisisitiza kuendelea kuwa
peke yake na kuifanya pombe ndiyo faraja
kubwa .
Coletha Raymond ‘ Koleta’ .
Akizungumza na mwandishi wetu kwa njia ya
simu mwanzoni mwa wiki hii , Koleta alisema
kamwe hawezi kusahau maumivu aliyopewa
na mchumba wake wa zamani baada ya
kumfuma zaidi ya mara moja na
kumsababishia maumivu makali moyoni.
“Niliumia sana, unajua nilikuwa bado binti
hivyo nilimpenda kwa moyo wangu wote,
alikuwa akiniambia maneno mengi mazuri na
matamu lakini mwisho wa siku nikaishia
kuumia, ” alisema Koleta.

1 comment:

.