Siku 7 tu baada ya shirika la Umeme Tanzania
(TANESCO) kutangaza kumalizika kwa mgao wa
umeme wa siku kumi kwenye baadhi ya mikoa,
Kaimu Mkurugenzi mtendaji Tanesco Felchesmi
Mramba
amethibitisha kwamba shirika lake linatarajia
kufanya biashara ya kuuza umeme nje ya
Tanzania.
Anakwambia ‘Uwezekano wa kuuza umeme nje
ya nchi upo, tunatarajia mwaka 2016 ndio
tutaanza kuuza manake kwa sasa ni kweli
hatuna umeme wa kutosha kuuza ila mwaka
2015 ndio Tanzania itaanza kuzalisha umeme
mwingi ambao ndio tutauuza 2016 baada ya
kujenga transmission lines za kutuunganisha na
majirani manake soko liko, Kenya na Zambia ni
miongoni mwa nchi ambazo hazina umeme wa
kutosha’
Bei ya umeme Tanzania iko chini sana
ukilinganisha na majirani zetu, yetu ni senti
11.5 za Kimarekani, Uganda ni 17.5, Kenya
ilikua 19 lakini juzi wameshusha na kuifanya
18.5 hivyo hata ukitulinganisha nao bado
Tanzania tuko chini kwenye bei.
Friday, December 6, 2013
EXCLUSIVE; TANZANIA KUUZA UMEME NCHI JIRANI?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Waniandikie cheki yangu kabisaa sio wanauza wakat mi sipat
ReplyDelete