Saturday, December 7, 2013

KUVUNJIKA KWA NDOA YA THEA, USHIRIKINA WATAJWA


Stori: Gladness Mallya na Hamida Hassan
SIKU chache baada ya ndoa ya mastaa
wawili wa filamu Bongo, Salome Ndumbagwe
Misayo ‘ Thea ’ na Michael Sangu ‘ Mike ’
kuvunjika, imedaiwa mambo ya kishirikina
yanahusika kwani mauzauza yalianza siku
nyingi zilizopita.
Thea na Mike siku ya ndoa yao.
Mtu wa karibu wa mastaa hao aliyeomba jina
lake liwekwe kapuni alidai kuwa mara kadhaa
wasanii hao wamekuwa wakikumbwa na
mambo ya ajabu yaliyoashiria kuwa ndoa yao
haina uhai.
“Unajua kwa nyakati tofauti pete za ndoa za
Thea na Mike ziliwahi kuwatoka kiajabu
vidoleni wakiwa chooni . Haikuwa jambo la
kawaida na wenyewe walishituka na kukosa
amani ,” alisema mtoa habari huyo.
Hata hivyo , wahusika wamekuwa wakiamini
kuvunjika kwa ndoa yao ni mipango ya
Mungu licha ya Mike kuhisi kuwepo kwa
nguvu za giza katika kuachana kwao .
“Mimi naamini kila linalotokea ni mipango ya
Mungu lakini katika hili mmh , napata
mashaka, ” alisema Mike .
Naye The alisema : Mungu hakupanga tu
tuendelee kuwa kwenye ndoa , kwa hiyo
limetokea na maisha yanaendelea . ”

1 comment:

.