LILE gari aina ya BMW X 6 alilokuwa
akitanulia mwigizaji Jacqueline Wolper
linaendelea kuoza katika yadi ya Majembe ,
Mwenge jijini Dar kutokana na kudaiwa
ushuru .
Jacqueline Wolper .
Taarifa ambazo Risasi Jumamosi limezipata
kutoka katika vyanzo tofauti , zimeeleza kuwa
hakuna uwezekano wa gari hilo kurudi katika
mikono ya Wolper kwani aliingizwa mkenge
tangu aliponunuliwa na aliyekuwa mpenzi
wake, Abdallah Mtoro ‘ Dallas ’ .
“Wolper aliingizwa mkenge tangu
aliponunuliwa lile gari , lilikuwa linadaiwa
ushuru sasa yeye bila kujua akaingizwa
mkenge na pedeshee Ndama na kisha mtego
wa kulinasa ukafanyika, Ndama huyohuyo
akaja kumgeuka akawa anaeneza uvumi
kuwa Wolper kaingizwa mkenge , ” kilidai
chanzo.
Gari aina ya BMW X 6 alilokuwa akitanulia
mwigizaji Jacqueline Wolper linaendelea
kuoza katika yadi ya Majembe , Mwenge jijini
Dar
Akizungumza na paparazi wetu hivi karibuni ,
Wolper aliweka bayana kuwa gari lile
alilonunuliwa kwa dola 130 , 000 ( zaidi ya Sh .
Mil. 170 ) kipindi penzi lake na Dallas
lilipokuwa likichanua , mwaka jana polisi wa
kimataifa ( Interpol ) kwa kushirikiana na
Mamlaka ya Mapato Tanzania ( TRA )
walilikamata kwa kudaiwa ushuru .
“Sina ujanja tena kwani hata mimi nilikuwa
sijaelewa kama linadaiwa lakini Ndama ndiye
aliyejua mchongo mzima , akaniingiza chaka .
Hadi sasa linaozea pale Majembe, sina jinsi,
namuachia Mungu ,” alisema Wolper na
kuongeza :
“Nilipolikabidhi Majembe na kuonesha
documents ( nyaraka ) zote, niliambiwa
nitalipata baada ya muda lakini mpaka leo
sijaambiwa lolote . Linaozea pale .”
Saturday, December 7, 2013
GARI LA WOLPER LAOZEA YADI DAR
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment