Saturday, December 7, 2013

MTOTO ALIYELELEWA NA MBWA AZIDI KUTESEKA


Stori: Denis Mtima na Chande
Abdallah,waliokuwa Mwanza
MTOTO Kulendya Rojason ( 3) ambaye siku za
nyuma aliwahi kuripotiwa na vyombo vya
habari kuwahi kulelewa na mbwa baada ya
wazazi wake kumtelekeza yeye na ndugu
zake, bado anazidi kuteseka kwa kukosa
msaada wa chakula .
Mtoto ( kulia ) wa aliyelelewa na mbwa .
Akizungumza kwa niaba ya mtoto huyo
nyumbani kwao , Nyerere B , Mabatini
Mwanza, dada wa mtoto huyo, Recho
Rojason ( 18) alisema kuwa mdogo wake
bado anateseka kwani hapati malezi ya
kutosha kutokana na maisha yao kuwa
magumu.
Baba wa mtoto .
Recho alisema kuwa , maisha yao yamekuwa
magumu baada ya mama yake kuwatelekeza
na kuolewa na mwanaume mwingine huku
akimwacha baba yao ambaye ametopea
kwenye ulevi na kushindwa kutoa msaada
wowote .
Recho ambaye ni hausigeli anayefanya kazi
kwa ujira mdogo maeneo ya Mwanza Mjini,
alisema wamekuwa wakipata fedha kidogo
kutoka Halmashauri ya Jiji ambapo hazikidhi
mahitaji yao na kuwaomba watu wajitokeze
kuwasaidia.
Nyumba anayoishi mtoto huyo .
Aliomba msaada wa kupata fedha kwa ajili
ya matibabu , masomo na malazi kwa kuwa
yote hayo ni mahitaji yao yeye pamoja na
wadogo zake watano akiwemo Kulendya .
Akizungumzia sakata hilo jirani anayeishi na
watoto hao , Chausiku Ibra alisema kuwa
watoto wa familia hiyo wamegeuka
machokoraa kutokana na huduma hafifu na
kuongeza kuwa mtoto wa mwisho ( Kulendya )
ndiye yupo hatarini zaidi .
“Huyu mtoto wa mwisho ndiye aliye hatarini
zaidi kwa kuwa tangu alivyokuwa mtoto
alikuwa akiletewa chakula na kutunzwa na
mbwa.
Mpaka anakuwa hivi ni jambo la kumshukuru
Mungu kwa kweli . Watoto hawa wanahitaji
msaada jamani , ” alisema jirani huyo.
Waandishi wetu walijionea , nyumba
wanayoishi watoto hao ambayo imeonekana
kuharibika kwa kiasi kikubwa sehemu za paa
na kuta jambo ambalo ni hatari kwa watoto
hao huku taarifa zikieleza kuwa , baba wa
watoto hao , Rojason Ernest amelazwa katika
Hospitali ya Rufaa ya Bugando akiuguza
nyonga baada ya kuanguka akiwa anatokea
kilabuni .
Kama umeguswa na unataka kuwasaidia
watoto hao , wasiliana nao kwa namba ya
jirani yao, Chausiku : 0767445683.

No comments:

Post a Comment

.