ANAITWA Graca Simbine Machel ni
Mmozambique ( Msumbiji ) . Kufuatia kifo cha
rais wa kwanza wa Afrika Kusini huru, Nelson
Mandela ( 95) kilichotokea usiku wa kuamkia
jana, Graca anakuwa mwanamke pekee
duniani kuwa mjane wa marais wawili
kwenye nchi mbili tofauti .
Marehemu Nelson Mandela ( kushoto) na
Graca Machel .
Mwaka 1975 hadi 1986 , Graca alikuwa mke
wa Rais wa Msumbiji , marehemu Samora
Moses Machel. Wakati huo, Graca alikuwa
waziri wa elimu na utamaduni wa nchi hiyo .
Baada ya kifo cha mumewe kilichotokea kwa
ajali ya ndege mwaka 1986 , Graca aliishi
mjane hadi mwaka 1998 ambapo alifunga
ndoa na Nelson Mandela akiwa rais wa
kwanza wa Afrika Kusini huru. Ni baada ya
Mandela kumtaliki mkewe wa pili , Winnie
Madikizele Mandela kwa madai ya kutokuwa
mwaminifu katika ndoa .
Kuanzia hapo mwanamama huyo alianza
kutambulika kwa jina la Graca Machel
Mandela.
Hata hivyo , Graca alishika nafasi ya u -first
lady wa ‘ Sauz ’ kwa mwaka mmoja tu , 1999
mumewe hakugombea tena urais .
Kifo cha mumewe kimempa ujane mwingine
unaodaiwa kutotokea duniani , kuolewa na
rais, rais kufa , kuolewa na rais mwingine
naye kufa .
HISTORIA YA GRACA KWA UFUPI
Graca alizaliwa Oktoba 17, 1945 katika Jimbo
la Gaza nchini Msumbiji .
Alipata elimu ya msingi jimboni humo , elimu
yake ya chuo kikuu aliipatia Lisbon, Ureno .
Ana watoto wawili, Malengani na Josina
aliowapata kwa marehemu Machel. Hakupata
mtoto kwa Mandela.
Saturday, December 7, 2013
MACHEL ; MJANE WA KIPEKEE DUNIANI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment