KLABU ya Gor Mahia ya Kenya haina presha na
kipa wake Ivo Mapunda na imesisitiza
kumuongezea mkataba baada ya kumalizika kwa
michuano ya Kombe la Chalenji.
Mapunda, ambaye mkataba wake unamalizika
mwezi huu, ndiye kipa namba moja wa
Kilimanjaro Stars ambayo inacheza robo fainali
dhidi ya Uganda leo Jumamosi mjini Mombasa.
Makamu Mwenyekiti wa Gor Mahia, David Kilo
alisema watamuongezea mchezaji huyo mkataba
na mpaka sasa wanajua ni mchezaji wao.
“Hakuna kilichobadilika mpaka sasa Ivo ni
mchezaji wetu na tunasubiri tu imalizike
michuano ya Chalenji tukae naye mezani tuingie
makubaliano mapya,” alisema David.
Kiongozi huyo alikiri kwamba wamesikia kwamba
kipa huyo amekuwa akiwindwa na timu nyingine
lakini wao wanaamini atasaini nao mkataba
mpya.
Simba imekuwa ikihusishwa na mpango wa
kumsajili kipa huyo ingawa ujio wa Yaw Berko
unaweza ukawashawishi kuachana naye. Ivo
ameonyesha kiwango kikubwa kwenye michuano
ya Chalenji inayoendelea na kuwa kikwazo kwa
washambuliaji wakorofi wa timu pinzani.
Kabla ya kutua Gor Mahia, Mapunda amewahi
kuzidakia klabu za Prisons na Yanga. Aliyewahi
kuwa kocha wa Stars, Marcio Maximo pia
alipenda kumpa nafasi Ivo dhidi ya makipa
wengine.
Tuesday, December 10, 2013
GOR MAHIA YAMKOMALIA KIPA IVO MAPUNDA-YASEMA HAENDI POPOTE BADO WANAMUHITAJI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment