Tuesday, December 10, 2013

HUU UGOMVI NA PREZZO NA HUDDAH UNAPOELEAKEA....!! AU NDIYO KUSAKA UMAARUFU...??


Uhasama mkali unaozidi kuchemka kati ya rapa
mbishi CMB Prezzo na 'msocialite’ Huddah
Monroe wameamua kuanikana wazi na kuzitoa
siri zao za ndani kwenye mtandao.
Tatizo nzima lilianza pale Huddah alipomkashifu
Prezzo kwenye akaunti yake ya Instagram
akimtaja kuwa mtu aliyeishiwa na anayependa
kudekezwa sana.
Kama kawaida yake 'king wa maBling’ alijibu
mpigo kwa kumwita Huddah kiruka njia
asiyejielewa na ambaye yupo tayari kutumiwa na
kila mtu.
Kipusa huyo naye hakuchoka kumjibu akisema
kwamba kheri kuwa kiruka njia kuliko kuwa mtu
wa kutegemea mamake hata katika umri
mkubwa kama wake Prezzo
Majibizano yalizidi kuwa makali huku wawili hao
wakitupiana cheche zaidi yenye soni kwenye
akaunti zao mbalimbali za mtandaoni ikiwemo
Twitter.
Letu ni jicho tu maana hatujui picha hii mbaya
kati ya wawili hawa itaishia wapi, au labda ndio
suala nzima la kusaka umaarufu.

2 comments:

.