Friday, December 13, 2013

HABARI MBAYA KWA MAN UNITED ! ROBIN VAN PERSIE NJE , KUKOSA MECHI 8


Straika wa Man United, Robin van Persie.
Straika wa Man United , Robin van Persie
atakuwa nje ya uwanja kwa muda wa mwezi
moja na kukosa mechi nane za timu yake
kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya
nyama za paja.
Mshambuliaji huyo alianza kupata maumivu
katika mechi dhidi ya Shakhtar Donetsk,
Jumanne iliyopita , maana yake ni kuwa
atakuwa nje ya uwanja mpaka Januari
mwakani.
Mechi ambazo atazikosa Van Persie ni:
Aston Villa , Desemba 15 , 2013
Stoke , Desemba 18, 2014
West Ham , Dec 21 , 2013
Hull, Dec 26, 2013
Norwich, Dec 28 , 2013
Tottenham, Jan 1 , 2014
Swansea, Jan 5, 2014
Swansea, Jan 11, 2014

No comments:

Post a Comment

.