Friday, December 13, 2013

IVO MAPUNDA NA DONALD MUSOTI WAJIUNGA RASMI NA SIMBA SC


KIPA Ivo Philip Mapunda, amesaini Mkataba
wa kujiunga na klabu ya Simba SC ya Dar es
Salaam ,akitokea Gor Mahia ya Kenya .Ivo
amesaini Simba SC, baada ya kung ’ ara
akiwa na kikosi cha Tanzania Bara
‘ Kilimanjaro Stars ’ katika michuano ya
Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na
Kati , CECAFA Challenge mwaka huu.
Ivo aliiongoza Kilimanjaro Stars kufika Nusu
Fainali ya Challenge baada ya kuwatoa
waliokuwa mabingwa watetezi Uganda ‘ The
Cranes’ kwa penalti 3- 2 kufuatia sare ya 2-2
ndani ya dakika 90, kipa huyo akicheza
mikwaju miwili .
Ivo alisema kwamba ameamua kusaini timu
hiyo yenye makao makuu mtaa wa Msimbazi
baada ya kuridhishwa na maslahi
aliyopewa. Ivo alisema kwamba Simba SC ni
timu kubwa na anaamini atafanya vizuri. Ivo
pia amewahi kuidakia Yanga SC.

No comments:

Post a Comment

.