Friday, December 13, 2013

JIDE AUGUA GHAFLA


Mwanamuziki mwenye jina kubwa katika
Bongo Fleva , Judith Wambura Mbibo ‘ Lady
Jaydee ’ hivi karibuni aliugua ghafla akiwa
nyumbani kwake Kimara - Temboni , Dar na
kukimbizwa katika Hospitali ya Primier Care
iliyopo karibu na nyumbani kwake.
Akizungumza na gazeti hili , ‘ hazibandi ’ wa
staa huyo ambaye pia ni meneja wake, Gadna
Habash ‘ Kapteini’ alisema kuwa ‘ waifu’ wake
huyo alipata maambukizi katika koo lake
hivyo akatumia dawa ambazo hazikustahili.
Judith Wambura Mbibo ‘Lady Jaydee ’
akichezea simuHospitali ya Primier Care .
Gadna alifunguka kuwa baada ya kutumia
dawa hizo zilimletea homa kali ndipo
walipomkimbiza katika hospitali hiyo na
kugundua kuwa alitumia dawa ambazo
hazikustahili kwa tiba ya koo hivyo walimlaza
na kumuanzishia dozi nyingine .
“Mwanzo hata sisi tuliogopa sana kwa
sababu alikuwa na homa kali lakini
tulipomfikisha hospitalini waligundua kuwa
alitumia dawa ambazo siyo tiba ya tatizo
lake ambazo ndizo zilimdhuru , lakini hivi
sasa yuko sawa na anaendelea na shughuli
zake, ” alisema Kapteini ambaye ni mtangazaji
wa kipindi cha Maskani cha Radio Times FM.

1 comment:

.