Friday, December 6, 2013

HII HAPA RATIBA KAMILI MPYA YA MAZISHI YA MADIBA


Rais Jacob Zuma ametangaza muda
mfupi uliopita kwamba mazishi ya
Nelson Mandela yatafanyika siku ya
Jumapili, Desemba 15 kijijini kwake
Qunu, katika jimbo la Eastern Cape.
Rais Zuma pia ametangaza siku 10 za
maombolezo kitaifa na bendera
zitapeperushwa nusu mlingoti katika
muda wote huo. Na ameitangaza siku ya
Jumapili ya Desemba 8, 2013 kuwa siku
maalumu ya kitaifa ya maombolezo na
kumkumbuka Madiba nchi nzima.
Tayari msisimko wa mazishi hayo
yanayotarajiwa kuwa ya kihistoria
umekamata dunia nzima, ambapo tayari
Rais Obama wa Marekani, mstaafu Bill
Clinto na Waziri Mkuu wa Uingereza
David Cameron ni baadhi tu ya viongozi
ambao wamethibitisha kushiriki.
Sala ya mazishi imepangwa kufanyika
katika uwanja wa Taifa wa  FNB
Desemba 10, 2013 jijini Johanesburg.
Mwili wake utawekwa jengo la serikali
liitwalo Union Buildings kuanzia
Desemba 11 hadi 13, kwa kupewa
heshima za mwisho, kabla ya kupelekwa
kijijini Qunu kwa mazishi
Uwanja wa Taifa wa michezo wa
Johannesburg ambako sala rasmi ya
Kitaifa ya mazishi itafanyika siku ya
Jumapili ya Desemba 10, 2013
Jengo la Union Buildinga ambapo mwili
wake utawekwa kwa ajili ya kupewa
heshima za mwisho kuanzia Desemba 11
hadi 13, 2013
Ulinzi mkali katika nyumba ya familia
ya Madiba kijijini kwake Qunu ambako
atapumzishwa katika nyumba yake ya
milele Desemba 15, 2013.

No comments:

Post a Comment

.