Friday, December 13, 2013

HII NI FUNGA MWAKA!


AISEEE ! Yameshuhudiwa matukio mengi ya
kamatakamata ya dadapoa kwa mwaka 2013
lakini hili ni funga mwaka.
Oparesheni Fichua Maovu ( OFM ) ya Global
Publishers kwa kolabo na polisi , safari hii
imefumua madanguro mengi yaliyojificha
vichochoroni na kwenye nyumba za kulala
wageni na kuibuka na mambo mengi ya
kushangaza.
Katika oparesheni hiyo maalum iliyofanywa
na OFM na polisi wa Kituo cha Buguruni , Dar ,
usiku mnene, mwanzoni mwa wiki hii ,
ilifanikiwa kuwanasa akina dada wanaouza
miili katika maeneo mbalimbali wakiwa na
wateja wao ambapo baadhi yao walitiwa
mbaroni.
MAENEO MENGINE
Ukiachilia mbali sehemu za madanguro hayo,
OFM ilitonywa kuwepo kwa baadhi ya gesti
zinazotumiwa na wanawake hao kama
madanguro kwa kuingiza na kubadili
wanaume asubuhi , mchana na usiku .
Oparesheni hiyo ilisafisha maeneo ya
Buguruni ambayo ni korofi kwa biashara hiyo
haramu ambapo baadhi yao walidai kuwa
wapo kwenye mishemishe za kusaka fedha
kwa ajili ya sikukuu ijayo ya Krismasi .
MENGI YABAINIKA
Katika upelelezi wetu, baadhi ya wanawake
walionaswa kwenye sekeseke hilo, ni
wachumba na wake za watu .
Baadhi ya watu waliokuwa karibu na maeneo
hayo, walisema imekuwa ni kero kwao kwani
uwepo wa wanawake hao maeneo hayo
huleta picha mbaya kwa jamii hasa watoto.
“Safi kabisa , nalipongeza sana jeshi la polisi
na OFM kuweza kuyabaini na kuyafanyia kazi
maovu haya, watoto wetu wamekuwa
wakishuhudia uchafu mwingi sana, ” alisikika
mama mmoja wa makamo .
MACHANGUDOA HAWA HAPA !
Wakizungumza na gazeti hili kwa nyuso za
huzuni, baadhi ya wanawake walionaswa
walikiri kuwa wachumba na wake za watu ila
kutokana na ugumu wa maisha wanalazimika
kujiingiza kwenye biashara hiyo .
“Jamani naombeni sana mniache, niko hapa
si kwa kupenda kwani ugumu wa maisha
ndiyo chanzo, mume wangu kwa sasa
hayupo, tafadhalini jamani , ” alisema mmoja
wao aliyejitambulisha kwa jina la mama
Batuli.
Wengine walisema si wake za watu lakini
wapo maeneo hayo kusaka fedha za
kujinasua na ukata kutokana na ukosefu wa
ajira hasa kuelekea kwenye kipindi hiki cha
msimu wa sikukuu .
WATEJA WAO SASA
Waandishi wetu waliendelea na upekuzi kwa
kuwapeleleza wanaume wateja walionaswa
nao kwa kuwauliza kulikoni wafanye hivyo
wakati mitaani kumejaa wanawake wengi
wastaarabu ambapo walifunguka kuwa
chanzo ni matatizo ya kindoa.
POLISI NA MSIMAMO WAO
Hata hivyo , jeshi la polisi kupitia Mkuu wa
Polisi wa Wilaya ya Kipolisi Buguruni ( OCD ) ,
Lucy Kakuru alisisitiza kuwa wataendelea
kupambana na biashara hiyo haramu hadi
suala hilo liishe maeneo hayo.

No comments:

Post a Comment

.