Friday, December 13, 2013

WEMA SEPETU ATIBUA TENA


BEAUTIFUL Onyinye , Wema Sepetu
ameendelea ‘ kutibua ’ hali ya hewa kwa
kukiuka maadili ambapo kwa mara nyingine
tena ametupia picha mtandaoni zikimuonesha
akiwa amevaa mavazi yaliyoacha wazi
baadhi ya sehemu nyeti za mwili wake .
Wema Sepetu .
Picha hiyo iliyopo kwenye baadhi ya
mitandao ya kijamii inamuonesha Wema
akiwa amevaa kiblauzi chenye matundu kiasi
cha kuifanya sidiria aliyovaa ionekane huku
sehemu nyingine zikiwa wazi .
Wakiizungumzia picha hiyo ambayo Wema
anaonekana akiwa na rafiki yake , Kajala
Masanja, baadhi ya wadau wamesema
msanii huyo anaonekana kujisikia raha sana
sehemu zake kuwa wazi.
“Mh! Huyu Wema na hivi vivazi vyake vya
nusu utupu hajambo , sijui anajisikiaje kuvaa
vile… hata kama atasema ni kutokana na hali
ya joto lakini hii sasa imezidi , huko ni
kuwatega wanaume , ” aliandika mdau mmoja
aliyejitambulisha kwa jina la Mwanaidi .

1 comment:

.