Tuesday, December 10, 2013

HIKI NDICHO WALICHOZUNGUMZA MASUPERSTAR WA BONGO KUHUSU SAKATA LA KUFANYA NGONO KINYUME NA MAUMBILE


Na Mwandishi Wetu
MADAI yameibuliwa kwamba asilimia 90 ya
warembo mastaa wanajihusisha na mchezo
mchafu wa mambo ya Pwani.
Mastaa wawili, Baby Madaha ambaye ni
mwanamuziki pia muigizaji na mtangazaji Lulu
Mathias Semagongo ‘Aunty Lulu’ ndiyo
waliolifichulia Uwazi wiki iliyopita.
Lulu alisema: “Mastaa wengi wakiambiwa
watakataa lakini wana tabia mbaya, hivi sasa
wanaona ndiyo fasheni.
“Hata wanaume kama mwanamke anakuwa
mgumu kwenda kinyume, anamuona mshamba,
tena wakati mwingine anakwambia mbona
mwenzako anatoa.”
Lulu alipoulizwa kama yeye amewahi kujihusisha
na mchezo huo alijibu: “Mimi sipendi kabisa, ila
iliwahi kunitokea mara moja kipindi nilipokuwa
na bwana wangu wa Kinzanzibari.
“Kwa kweli ni mateso makubwa. Kwanza yule
mwanaume alinibaka, haikuwa ridhaa yangu na
kunitenda hivyo nilimuacha. Nawaomba wengine
waelewe kuwa ni jambo baya. Binafsi sitakuja
kufanya katika maisha yangu yote.”
Lulu aliendelea kusema: “Mimi nina orodha ndefu
ya mastaa wanaojihusisha na tabia hiyo,
siwataji kwa sasa lakini zaidi ya asilimia 90.
Unajua hivi sasa hata wanaume wanaotendwa
mchezo mchafu ni wengi ndiyo maana
wanawake wanaamua kuachia ili wasizidiwe kete
na wanaume mashoga.”
Baby alisema: “Wanaojihusisha ni mastaa tena
wenye majina makubwa na mamisi maarufu.
Mara nyingi nawasikia wakizungumza hata
wakilewa, wanaeleza kinagaubaga kuhusu
michezo yao.
“Yaani ni noma, mbele ya fedha tena, watu
wanakubali kwa tamaa zao. Mimi mwenyewe
nilishaambiwa kuwa ni poa sana lakini moyo
umekuwa mzito. Nashukuru sijawahi kuambiwa
na mpenzi wangu yeyote kufanya hivyo.”
Mbali na hao, mastaa wengine waliozungumza
na gazeti hili walikiri kukithiri kwa tabia hiyo na
kutoa maoni yafuatayo;
MAIMARTHA JESSE
Anajulikana pia kama Oprah wa Bongo, alisema:
“Wengi wanafanya hicho kitendo kwa tamaa na
mihangaiko ya maisha. Kwangu mimi siwezi
kufanya, kina athari kubwa kiafya na naomba
watu wajue hilo.”
JULIET WILLIAM
Mshindi wa taji la dunia la Miss Progress
International, pia Miss Tanzania namba tatu
mwaka 2009, alisema: “Mtu anayefanya kitendo
hicho kwangu hana thamani, hicho kitendo siyo
kizuri kwani kinakwenda kinyume na matakwa ya
Mwenyezi Mungu.”
UMMY WENSLAUS ‘DOKII’
Staa huyo wa filamu alisema: “Watu wanaofanya
kitendo hicho bila shaka watakuwa na matatizo
ya akili. Wanatembea chini ya laana.”
MAUNDA ZORRO
Mwanamuziki huyo alisema: “Mtu anayefanya
mapenzi kinyume na maumbile hajui maadili ya
Mwafrika. Mwanaume anayemtamkia mwanamke
kuhusu kitendo hicho ujue hana malengo naye,
anataka tu kumchezea.”
JACQUELINE PENTZEL
Alisema: “Aku, mimi sijawahi kufanya hayo
mambo, ni dhambi mbele ya Mungu na
wanaofanya pengine akili zao ni pungufu.”
COLETHA RAYMOND
“Sipendi kitendo hicho, kama ningekua na mume
anayependa kufanya mchezo mchafu
ningemwacha haraka sana.”
STARA THOMAS
“Wanaofanya tendo la ndoa kinyume na
maumbile hawajui thamani ya utu wao, kitendo
hicho ni cha kijinga na ni ushamba. Wahusika
wakuu wanatakiwa kufikiri vizuri juu ya jambo
hili kwani hushusha thamani ya utu.”

2 comments:

.