Muigizaji wa filamu, Irene Uwoya amesema
kupitia kipindi chake cha Paradise ambacho
husaidia kuzifanyia ukarabati nyumba za
Watanzania zilizo na hali duni, amesema kipindi
hicho kimemfanya aione picha halisi ya jinsi
Watanzania wengi wanavyoishi katika umaskini
mkubwa.
Akiongea na mwandishi wetu, Irene amesema ni
ngumu kuyajua maisha ya mtu umwonapo
barabarani lakini ukienda anakoishi ndiko
utakapoujua ukweli.
“Nimegundua kwamba asilimia kubwa ya
Watanzania wanaishi katika mazingira magumu,
mabaya sana kuliko unavyotegemea,”amesema
Irene. “Unaweza ukakaa na mtu unapiga naye
story, kumbe kwake anakoishi ana maisha
magumu kwelikweli,”ameongeza.
“Kwahiyo mimi navyotembea hivi nakutana na
vitu vingi na nimejifunza mengi. Mimi nikikaa
kwangu naona niko sawa, wengine wanakuwa
hawana hata sehemu ya kwenda choo, mtu
akitaka kwenda chooni anachimba shimo kwa
jembe. Nimejifunza vitu vingi ambavyo nilikuwa
sivijui vinaendelea katika hii nchi.
Akiongelea changamoto za kipindi hicho, Irene
amesema wapo watu wamekuwa wakimpigia
simu na kumponda kuwa ameacha kujenga kwao
na ameamua kusaidia watu wasio ndugu zake.
Changamoto nyingine ni kukutana na watu
wanaojifanya wanashida kumbe ni wasanii tu.
“Kuna nyumba moja tulienda yule mama
akaelezea mpaka akalia lakini kumbe sinema tu,
hana matatizo wala nini,” amesema Irene.
Ameeleza kuwa wakati mwingine hukutana na
watu wenye matatizo makubwa ambayo
wakimuelezea hujikuta yakimgusa kiasi cha
kumliza na kushindwa kurekodi kipindi.
“Mara nyingi kila nikienda sehemu unakuta mtu
ananihadithia mpaka nashindwa kushoot
machozi yananitoka, yaani kiukweli nakuwa
naumia. Karibia scenes kibao nashindwa kushoot
sababu ya hiyo.”
Friday, December 13, 2013
IRENE UWOYA "NIMEGUNDUA WATANZANIA WANAISHI MAISHA MAGUMU SANA KULIKO UNAVYOTEGEMEA"
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Ndo umejuaaa atiii
ReplyDelete