Friday, December 13, 2013

RIHANNA AANDIKA HISTORIA NYINGINE KUBWA KIMUZIKI


Rihanna amefanikiwa kuandika historia nyingine
kimuziki kufuatia wimbo alioshirikishwa Eminem,
Monster kuwa wimbo wake 13 kukamata nafasi
ya kwanza kwenye chart za Billboard.
Akiwa na nyimbo 13 zilizokamata nafasi ya
kwanza, amewazidi Madonna, Stevie Wonder
na Whitney Houston na amefungana na
hayati Michael Jackson.
Wanaoongoza kwa kuwa na nyimbo nyingi
zilizoshika nafasi ya kwanza ni the Beatles
walioingiza nyimbo 20 na kufuatiwa na
Mariah Carey mwenye nyimbo 18.

No comments:

Post a Comment

.