Friday, December 13, 2013

Niyonzima, Kiiza waanza filamu zao, hawajulikani walipo


Khadija Mangwai na Hans Mloli
WACHEZAJI wawili wa kimataifa wa Yanga,
Haruna Niyonzima na Hamis Kiiza
wameshindwa kutua nchini kujiunga na
wenzao kwa ajili ya maandalizi ya mzunguko
wa pili wa Ligi Kuu Bara .
Wawili hao ambao walikuwa kwenye timu zao
za taifa katika Michuano ya Kombe la
Chalenji , wamekuwa na rekodi ya kuchelewa
kujiunga na wenzao pindi wanapoondoka
kwenda kwenye nchi zao, hivyo hii inaweza
kuwa ni mwendelezo wa ‘ filamu ’ zao hizo .
Ilielezwa kutoka ndani ya klabu hiyo kuwa ,
walikuwa wakitarajiwa kuwasili nchini juzi
Jumatano lakini mpaka jana asubuhi pia
hawakuwepo kwenye mazoezi ya timu hiyo
yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Bora jijini
Dar es Salaam.
Mtu wa ndani wa Yanga aliliambia gazeti hili
kuwa , walitakiwa kuwasili Jumatano lakini
mpaka jana haikujulikana watawasili lini kwa
kuwa pia namba zao za simu hazipatikani .
“Sasa viongozi wenyewe hawajui nini
kinaendelea hapo katikati , ” alisema mtu
huyo.
Alipoulizwa juu ya suala hilo, msemaji wa
Yanga, ambaye amekuwa na mbwembwe
nyingi zisizo za msingi kila anapoulizwa
masuala mbalimbali ya klabu yake hiyo ,
Baraka Kizuguto , alisema : “Muulizeni kocha
( Ernie Brandts ) yeye ndiye anaweza kujua,
sawa , mimi ni msemaji lakini siyo nasema
kila kitu .”

No comments:

Post a Comment

.