Monday, December 16, 2013

Mkenya atishia kuwakata posho Boban, Santo


WACHEZAJI watatu wa Coastal Union,
huenda wakakumbwa na adhabu ya kukatwa
posho zao au kusimamishwa kutokana na
kuchelewa kuripoti mazoezini .
Wachezaji ambao watakumbwa na adhabu
hiyo ni Juma Nyosso , Haruna Moshi ‘ Boban’
na Jerry Santo .
Akizungumza na Championi Jumatatu, Kocha
wa Coastal , Mkenya , Yusuf Chipo , alisema
Boban na Nyosso walitarajiwa kutua Tanga
jana Jumapili na Santo haijajulikana atawasili
lini , wakati wenzao tayari wameshaanza
maandalizi ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu
Bara tangu juzi .
Kocha huyo anayesisitiza suala la nidhamu
kwenye kikosi chake , alisema wachezaji hao
watakatwa kulingana na jinsi walivyochelewa.
“Lazima niwape adhabu kwa kuwa
hawakuwa na ruhusa maalum kutoka
kwangu , nitaangalia na adhabu za klabu
zinasemaje mtu akichelewa kazini , sipendi
nidhamu mbovu kwenye kikosi changu,
nataka wote tuwe sawa ,” alisema Chipo.

No comments:

Post a Comment

.