Ivo Mapunda ambae ni kipa wa sasa wa timu ya
taifa akiwa amechukua headlines za karibuni
kutokana na alichofanya
kwenye mashindano CECAFA, amezungumza
kuhusu stori nyingi Magazetini Tanzania kwamba
amejiunga na club ya Simba tayari huku mengine
yakisema amejiunga kwa Rav 4.
Kwenye Sports Extra ya Clouds FM, Ivo
amesema ‘sijaona karatasi yoyote ambayo
inanifanya mimi niweke saini yangu au kuongea
na kiongozi yeyote wa Simba mpaka sasa ila
tumekua tu tukiongea kwa simu kwamba
watakuja lakini bado hatujakaa meza moja
kuongea’
Ivo ambae amekua akicheza soka la kulipwa
huko Kenya hivi karibuni, kwenye sentensi ya pili
anasema ‘Mpira ndio kazi yangu, ndio maisha
yangu, sehemu yoyote ile nitakua tayari kama
tutakubaliana vizuri hasa kwenye maslahi…
popote mimi nacheza’
Jibu alilolitoa baada ya kuulizwa kama ni kweli
ameongezewa mkataba wa mwaka mmoja na
club yake ya Gor Mahia ya Kenya ni hili…. >>>
‘hapana, bado ila nimetoka kuongea na kiongozi
wa club ameniambia tukimaliza mechi kesho
ndio tukae tuongee, mimi nakaribisha
mazungumzo kwa club yoyote ile ambayo
itahitaji niichezee, itakayoonekana ina maslahi
ndio nitajiunga nayo’
Thursday, December 12, 2013
KAULI YA IVO MAPUNDA KUHUSU TETESI ZA KUSAJILIWA NA SIMBA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment