Na Khatimu Naheka
HALI ya mazoezi ya kikosi cha Yanga
imegeuka kuwa kama vita kali , sababu
kubwa ikitajwa kuwa ni kutaka mafanikio
katika mechi ya Mtani Jembe dhidi ya watani
wao Simba.
Juzi jioni kwenye Uwanja wa Bora uliopo
Kijitonyama jijini Dar , mazoezi ya kikosi hicho
yalionekana mithili ya wachezaji wa jeshi ,
ambapo nguvu nyingi na ufundi vilishamiri
kiasi cha kuwafanya mashabiki wa timu hiyo
kuguna wakihofia nyota hao kuumizana .
Licha ya hali hiyo kuwa ya kukamiana katika
mazoezi hayo yaliyoshuhudiwa na Championi
Jumatano , kocha wa kikosi hicho, Ernie
Brandts , hakuonyesha kujali hali hiyo ambapo
alizidi kuwasisitiza wachezaji wake kukaba
kwa nguvu huku nyota hao nao wakiongeza
juhudi katika hilo na kuvaana mara kwa
mara.
Mara baada ya mazoezi hayo, Championi
Jumatano lilizungumza na Brandts raia wa
Uholanzi , ambaye alionyesha kufurahishwa
na hali hiyo akisema lengo kubwa ni kutaka
kuwa sawa kabla ya mchezo huo wa Mtani
Jembe, utakaopigwa Jumamosi ya Desemba
21, kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar .
“Bila shaka nataka hali hiyo kuongezeka
zaidi , nimekuwa nikiwasisitizia suala la
ukabaji mara tu tunapopoteza mpira
na kucheza kwa nguvu kama hivi .
“Ukweli kama tunataka kushinda mchezo
dhidi ya Simba, tunatakiwa kucheza kwa
nguvu na kasi namna hii ,” alisema Brandts
Thursday, December 12, 2013
Simba yachafua mazoezi Yanga
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment