WACHEZAJI wa kimataifa wa Yanga, Mbuyu
Twite na Didier Kavumbagu , wamelivaa
Shirikisho la Soka Tanzania ( TFF ) kwa
kusema kuwa kusajili wachezaji watatu wa
kimataifa siyo chachu ya kuongeza viwango
vya wachezaji Bongo.
TFF imetangaza kuwa ifikapo msimu wa
2014/2015 kutakuwa na wachezaji watatu wa
kimataifa watakaotakiwa kucheza kwenye ligi
na siyo watano kama ilivyo hivi sasa .
Wakizungumza na Championi Jumatatu kwa
nyakati tofauti , wachezaji hao walisema
kupunguza idadi ya wachezaji wa nje siyo
kigezo cha kuweza kukuza soka la Tanzania ,
badala yake wachezaji wenyewe wanatakiwa
kujua wajibu wao kwa kujituma kuhakikisha
soka linasonga mbele .
“Unajua kupunguza idadi ya wachezaji wa
kimataifa siyo sababu ya kukuza soka la
Tanzania ! Sanasana litazidi kudidimia kwa
kuwa wachezaji wa nje ndiyo wanaoleta
changamoto ya wachezaji wa ndani
kujituma , ” alisema Twite .
Kwa upande wake Kavumbagu , alisema :
“Ukitaka soka liweze kukua , ni vyema kuwa
na wachezaji mchanganyiko, mfano mzuri ni
ligi ya Uingereza kwani kuna wachezaji wengi
wanaotoka nje lakini soka lao linazidi kukua
kila siku .
“Hata TP Mazembe wenyewe wana wachezaji
15 wa kigeni , ona timu yao inavyokuwa nzuri ,
kuondoa wachezaji wa kimataifa ni sawa na
kudidimiza soka , kinachotakiwa wachezaji
wenyewe wa hapa waweze kujituma ipasavyo
kwa kupata changamoto kutoka kwa wageni
ili kupata wachezaji wazuri hapo baadaye. ”
Monday, December 16, 2013
Kavumbagu , Twite waipinga TFF
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment