.
Kiungo wa Arsenal Jack Wilshere huenda
akaingia matatani baada ya kuwaonyesha
mashabiki wa Man City ishara ya matusi kwa
kidole chake sekunde chache baada ya mchezo
ambao Arsenal ilifungwa 6-3 kumalizika.
Wilshere akiwa anaonekana kukerwa na kelele
za mashabiki hao ambao walionekana kuimba
nyimbo za kumdhihaki aliwaonyesha kidole cha
kati ishara ambayo hutafsiriwa kama tusi
sehemu mbalimbali duniani.
Kutokana na kitendo hicho Wilshere yuko
hatarini kukumbwa na rungu la chama cha soka
cha England FA ambao kwa vyovyote
watalifanyia uchunguzi tukio hilo kabla ya
kulifanyia maamuzi.
Mara nyingi wachezaji wanaofanya kosa kama
hilo hukumbana na hatua za kinidhamu ikiwemo
kutozwa faini pamoja na kupewa adhabu ya
kufungiwa mechi kati ya mbili na tatu.
Hii itakuwa mara ya pili kwa mchezaji huyo
kuingia matatani baada ya kupigwa picha akiwa
anavuta sigara ndani ya klabu ya usiku huko
London wiki chache zilizopita .
Wachezaji kadhaa akiwamo David Beckham na
Luis Suarez wamewahi kukumbana na adhabu
tofauti baada ya kufanya kosa kama hilo.
Sunday, December 15, 2013
KIDOLE CHA KATI KUMGHARIMU KIUNGO WA ARSENAL "JACK WILSHERE"........
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment