Mchekeshaji maarufu Kingwendu anatuhumiwa
kumtapeli mtayarishaji wa filamu za kitanzania
‘Bongo Movies’ ambaye pia ni mshindi wa tuzo
za ZIFF, Bondi.
Akiongea kupitia kipindi cha Filamonata cha
100.5 Times Fm, kinachoongozwa na Monalisa
na mama yake ‘Natasha’, Bondi amesema kuwa
alimlipa pesa mchekeshaji huyo ili aweze kuigiza
kwenye filamu yake na kusaini mkataba, lakini
alipotea na kuelekea Msumbiji huku simu yake
ikiwa haipatikani.
“Nilimpa fedha ya advance akachikichia moja
kwa moja kumbe ana shows zake anaenda
kufanya huko Mozambique. Kwa hiyo imefika
siku ya kufanya filamu ambapo nilikuwa nashuti
mimi, Kingwendu hayupo na siku sita amezima
simu haipatikani.” Amesema Bondi.
Lakini kukosekana kwa Kingwendu kulimpa
shavu mchekeshaji mwenzake Bambo,
“Nikaamua nifanye option B, Option B niliyofanya
nikamtafuta Bambo nikaongea naye, nikaelewana
naye vizuri na tukafanya kazi.” Ameeleza
producer Bondi.
Naye Kambarage wa kampuni ya usambazaji wa
filamu ya Steps Entertainment, amesema kwa
kuwa Kingwendu amevunja mkataba na
kumuingizia Bondi gharama za ziada, kampuni
ya Steps imepanga kuongea na Kingwendu na
endapo ataenda kinyume watamfungulia
mashitaka ili iwe fundisho kwa wasanii wenye
tabia kama yake.
Filamonata inakuwa hewani kila Jumapili
kuanzia saa 5 kamili asubuhi hadi saa 7 mchana
kupitia 100.5 Times Fm.
Tuesday, December 10, 2013
KINGWENDU AGEUKA TAPELI AKIMBILIA MSUMBUJI NA MKWANJA WA DIRECTOR
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
tatizo wasanii njaa
ReplyDeleteHahahaha sio mbaya msanii kufanya usanii hahaha kingwendu anaigiza hapo
ReplyDeletehiii ndo bongo dar.
ReplyDeletehapa dar waweza kuwa mjanja lakin ukaitwa fala tu
ReplyDelete