“Ray ananifitini kwa sababu alinitongoza
nikamkataa“Nora
Muigizaji wa kike aliyefanya vizuri kupitia kundi la
Kaole Sanaa Group, Nuru Nassoro aka Nora
amedai kuwa amekuwa akifanyiwa fitina na
muigizaji mwenzake Vicent Kigosi aka Ray kwa
kuwa aliwahi kumtaka kimapenzi akamkataa.
Nora amefunguka kupitia kipindi cha Filamonata
cha 100.5 Times Fm na kudai kuwa Ray
amekuwa akimbania hata kwenye baadhi ya
makampuni ambayo anapeleka kazi zake.
“Mpaka kwenye kampuni ambayo nimepeleka kazi
nimeshawahi kusikia wanasema, wakaniahidi
sana mpaka nikawakubalia walichokuwa
wanataka wao. Lakini yeye (Ray) alitanguliza
movies zake, akasema ana movie zake sijui kitu
gani..” amelalamika Nora.
Ameeleza kuwa Ray amewahi kumbania kufanya
kazi na marehemu Kanumba, na hata Mtitu
sababu ikiwa ile ile kumkataa kimapenzi.
“Alishawahi..kitu ambacho kwangu kimeshawahi,
sasa mimi sijui yeye ni alivyo au kwangu..ila
mimi alinibania kwa sababu nilikuwa simtaki,
akaniharibia kwa Mtitu. Kanumba kipindi kile
alikuwa anamsikiliza sana Ray, akamwambia
asifanye kazi na mimi. Hata Kanumba alikuwa
ameelewana na mimi Ray akamwambia ‘achana
naye’.” Nora ameiambia Filamonata.
Amedai kuwa wanaume wengi katika tasnia ya
filamu wanamekuwa wanawanyanyasa wanawake
kwa kuwata kimapenzi, na kwamba inakuwa ni
mambo ya ndani ambayo sio rahisi kufahamika.
“Ikitokea hivyo inakuwa ni mambo ya ndani sana
kiasi kwamba hata mwenzako anakwambia
kwamba utaona kama utaendelea kuwa flani.”
Nora amefunguka.
Nora amedai kuwa ana kazi nyingi lakini
ameshindwa kuziingiza sokoni kwa sababu ya
kubaniwa.
Hata hivyo Nuru Nassoro aka Nora amesema
ameshasamehe na anaendelea na kazi zake.
Tuesday, December 10, 2013
Ray ananifitini kwa sababu alinitongoza nikamkataa“Nora
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Hliiiiih huyu naeee aaah
ReplyDeletekaona kapotea ktk game ndo anaongea cku zote ulikuwa wapi kusema?hebu kitulize!
ReplyDeleteKazi sna funguka mdada
ReplyDeleteMambo ya ray
ReplyDelete