Tuesday, December 10, 2013

Talib Hilal atupa neno kwa kocha Simba SC


KOCHA wa zamani wa Simba, Talib Hilal,
amesema kocha mpya wa Simba, Zdravok
Logarusic , ana mtihani mkubwa wa
kuhakikisha anaipa mafanikio timu hiyo ,
ingawa amekiri kuwa ni bonge la kocha . Loga
amejiunga na Simba kwenye dirisha dogo la
usajili ambapo amesaini mkataba wa miezi
sita.
Akizungumza na Championi Jumatano , Hilal
ambaye aliwahi kuwa mchezaji wa timu hiyo ,
alisema Loga anahitaji kupewa ushirikiano
mkubwa kutoka kwa wanachama na
mashabiki lakini pia ana mtihani mkubwa
kuhakikisha anawapa kitu ambacho
wanakitaka.
Pia alisema ni vyema walivyomchagua
Selemeni Matola kama kocha msaidizi kwa
kuwa anawajua vyema vijana waliopo Simba
hivyo atasaidiana vizuri na kocha huyo
Mzungu .
“Kocha huyu kwanza lazima nimpe heshima
yake, ni mzuri lakini ana mtihani mkubwa
sana wa kuirudisha Simba ile iliyokuwa
ikitesa , nafikiri anahitaji kupewa kwanza
ushirikiano ili afanikishe malengo
aliyojiwekea, ” alisema Hilal.

No comments:

Post a Comment

.