SIMBA ya Kocha Zdravok Logarusic ‘ Loga ’
imeanza kazi rasmi kwa ushindi wa mabao
3-1 , baada ya jana kuifunga KMKM ya
Zanzibar katika mechi ya kirafiki kwenye
Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam .
Simba ambayo ipo chini ya kocha huyo
aliyeiongoza timu hiyo kwa mara ya kwanza ,
ilikuwa na mabadiliko kadhaa ambapo pia
ilianza mchezo huo kwa kasi huku mwalimu
huyo raia wa Croatia akiwa mkali kwa
wachezaji wake alioona wanacheza kinyume
na maelekezo yake .
Akizungumza mara baada ya mechi hiyo ,
Loga alisema : “Nilihitaji kuangalia wachezaji
wangu kabla ya mechi ya Yanga ( Jumamosi
ijayo ) na ndiyo maana nikafanya mabadiliko
kadhaa, hii imenisaidia kujua tulipofikia ,
kambi ambayo tunaenda kuiweka Zanzibar
itatusaidia zaidi .”
Kuonyesha kuwa hana utani kazini , Loga
ambaye ni kocha wa zamani wa Gor Mahia ,
alizungumza na straika wake , Betram
Mwombeki mara kadhaa kuwa atumie akili
katika maamuzi yake , alipoona bado
hatekelezi kile anachomwambia, akamtoa
katika dakika ya 30 na kumuingiza Amissi
Tambwe.
Loga alikuwa hatulii kwenye benchi ,
aliongeza ukali na kuwasisitiza wachezaji
wake kuwa makini, ambapo pia Tambwe naye
alikutana na ‘ dhahama ’ kama aliyoipata
Mwombeki kutokana na kumpigia kelele mara
kadhaa kisha kumtoa katika dakika ya 86 na
nafasi yake kuchukuliwa na Issa Abdallah .
Said Ndemla ndiye aliyeanza kufungua
ukurasa wa mabao kwa kufunga katika
dakika ya 11 kwa shuti kali ndani ya 18
baada ya kupokea pasi kutoka kwa
Mwombeki. Bao la pili lilifungwa na
Christopher Edward dakika ya 16 kwa
kumchambua kipa wa KMKM , Mudathir
Khamis baada ya kupata pasi kutoka kwa
Omar Salum.
Kuelekea mapumziko katika dakika ya 40,
straika wa KMKM , Ally Ahmed alipiga shuti
kali ambapo Berko alipangua kisha mabeki
wake wakaokoa .
Henry Joseph ambaye ndiye aliyekuwa
nahodha wa Simba alifunga bao la tatu kwa
penalti katika dakika ya 87 iliyopatikana
baada ya Issa Abdallah kuchezewa rafu na
Khamis Ally wa KMKM .
Wakati Simba ikiendelea na mchezo , Kocha
wa Yanga, Ernie Brandts alikuwepo uwanjani
huku akionekana kuwa makini na kuandika
vitu kadhaa kwenye karatasi yake.
Bao la KMKM lilifungwa na Shiboli kwa njia
ya penalti katika dakika ya 76 baada ya
Omari kumchezea vibaya Iddi Kambi.
Simba walipunguza kasi katika dakika 10 za
mwisho na kuonekana kama wamechoka .
Henry aliyezoeleka kucheza nafasi ya kiungo,
jana alicheza nafasi ya beki wa kati namba
tano akiwa na Joseph Owino wakati Issa
Rashid ‘ Baba Ubaya’ ambaye kawaida
anatumika nafasi ya beki wa kushoto ,
alitumika nafasi ya winga wa kushoto .
Simba: Yaw Berko , Haruna Shamte, Omar
Salum, Joseph Owino , Henry Joseph, Jonas
Mkude, Uhuru Selemani, Said Ndemla ,
Edward Christopher , Betram Mwombeki na
Issa Rashid ‘ Baba Ubaya’ .
Monday, December 16, 2013
Simba ya Logarusic ni moto chini
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment