Mlezi wa Simba, Rahma Al Kharoosi ' Malkia
wa Nyuki ' .
MLEZI wa Simba, Rahma Al Kharoosi, ametua
jijini Dar es Salaam akiwa kwenye ndege
kubwa yenye uwezo wa kubeba watu 150 ,
lakini yeye akiwa ndiye abiria pekee ndani ya
ndege hiyo .
Rahma , maarufu kama Malkia wa Nyuki ,
ametua na ndege hiyo aina ya Airbus 320
inayomilikiwa na Serikali ya Oman na
anaitumia yeye kupitia cheo chake cha Balozi
wa Heshima wa Oman nchini Morocco .
Ndege hiyo ilikuwa imebeba watu 17 , kati ya
hao 16 ni wafanyakazi ndani ya ndege
ambao ni daktari mmoja , walinzi wanne ,
waliobaki ni marubani na wahudumu .
Akizungumza dakika chache kabla ya
kuondoka nchini jana , saa 10 alfajiri , Malkia
wa Nyuki alisema alishuka nchini kwa ajili ya
mapumziko ya siku moja , pia kuzungumza na
baadhi ya viongozi wa Simba.
“Nimepita tu , tumepumzika kidogo hapa na
baada ya hapo ninakwenda Comoro kwa ajili
ya kuzungumza na kumchukua Rais wa
Comoro.
“Lakini wakati wa mapumziko , nimepata
nafasi ya kuzungumza na baadhi ya viongozi
wa Simba kuhusiana na mwenendo wa timu
kwa hivi sasa .
“Kwa sasa namaliza majukumu yangu kikazi
halafu nitarudi tena safari nyingine nchini
kwa ajili ya kuendelea na mazungumzo na
viongozi wenzangu wa Simba ili tujue
tunaweza kufanya nini kuendelea kurekebisha
mambo, ” alisema .
Kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Julius Nyerere ( JNIA) , Malkia wa Nyuki
alisindikizwa na mwanaye Fatma, maarufu
kama Nyuki Mtoto na watu wengine wawili.
Baada tu ya yeye kupanda ngazi za ndege
hiyo , walinzi na wafanyakazi waliokuwa nje
ya ndege hiyo nao waliingia na ikaanza
safari kwenda Comoro .
Monday, December 16, 2013
Kufuru , ndege ya watu 150, Malkia wa Nyuki apanda peke yake
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment