Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete kwenye mazishi
ya Rais wa kwanza wa Afrika Kusini Nelson
Mandela leo huko Qunu, Eastern Cape nchini
Afrika Kusini, imewakumbusha Waafrika ukaribu
wa kihistoria uliopo kati ya Tanzania na Afrika
Kusini.
Katika hotuba hiyo iliyosifiwa na Waafrika wengi,
Kikwete aligusia jinsi ambavyo Afrika Kusini haipo
peke yake kwenye maombolezo ya shujaa wao,
Mandela.
“Watu wa Tanzania wangependa mjue kuwa
hamko peke yenu. Watakuwa nanyi katika kipindi
hiki cha maombolezo na baada ya hapa. Potezo
lenu ni potezo letu. Alikuwa kiongozi wetu, shujaa
wetu, mfano wetu, baba yatu kama alivyo kwenu.
Watu wa Tanzania wamepoteza rafiki mkubwa.
Komredi mkubwa jeshi,” alisema Kikwete.
Katika hotuba hiyo pia, Kikwete alikumbushia jinsi
Nelson Mandela alivyoacha viatu vyake jijini Dar
es Salaam mwaka 1962 ambavyo vilirudishwa
kwake alipokuja kuwa rais. Ulikuwa ni muendelezo
mwingine wa kuvutia wa ujio wake Tanzania
mwaka 1962,” alisema.
“Katika kuufanya ujio wake kuwa makini, hakukaa
kwenye hoteli. Alikaa kwenye nyumba ya Cyril
Swai. Alipoondoka, aliacha viatu vyake kwa
matumaini kuwa akiwa anarudi angevipitia viatu
vyake Bahati mbaya hakupitia Dar es Salaam
tena sababu aliporejea Afrika Kusini alikamatwa
na kukaa jela miaka 27. Bahati nzuri, familia ya
Swai ilivitunza viatu vyake na mwaka 1995, viatu
hivyo vilirudishwa kwake.”
Mjane wa Swai, Vicky alikuwepo pia kwenye
mazishi ya Mandela
fungua hapa uangalie hiyo hotuba
https://www.youtube.com/watch?v=IDYpZEee7Sw&feature=youtube_gdata_player
No comments:
Post a Comment