SIYO habari tena , kwani dunia nzima inajua
kuhusu kifo cha shujaa wa Afrika, nembo ya
mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi ,
komredi aliyefungwa jela miaka 27 akitetea
usawa baina ya wananchi wa Afrika Kusini,
Nelson Rolihlahla Mandela .
Risasi Jumamosi , kwa msaada wa vyanzo
mbalimbali , linamulika kwa undani chanzo
hasa cha kifo cha Mandela , aliyefikwa na
mauti usiku wa kuamkia jana, Desemba 5,
mwaka huu akiwa na umri wa miaka 95.
Mandela akiwa na mkewe Graca Machel
( kushoto ) na mtalaka wake, Winnie
Mandela ( kulia ) .
Ripoti za ndani zaidi , zinabainisha kuwa afya
ya Mandela ilianza kuleta mushikeli tangu
akiwa kijana na kwa mantiki hiyo , sehemu
kubwa ya maisha yake alisumbuliwa na
maradhi.
UNDANI WA MARADHI YALIYOMUUA
Ripoti za wataalamu mbalimbali kuhusu afya
ya Mandela , kwa pamoja zinatoa majibu
kwamba chanzo cha maradhi ya mapafu
ambayo ndiyo hasa yaliyokatisha uhai wake
ni matokeo ya ukatili aliokuwa anafanyiwa
gerezani, kipindi akiwa mfungwa wa kisiasa.
Habari zinasema kuwa kufanyishwa kazi
ngumu bila kujali afya yake , kutopewa
matibabu ya uhakika na mazingira hatari
aliyoshurutishwa kuishi gerezani ni kichocheo
cha afya yake kuwa mgogoro tangu ujana
hadi kifo kilipomchukua.
“Alifanyishwa kazi za kupasua mawe , kipindi
hicho vumbi nyingi ziliingia mwilini , mahali
alipolala palikuwa na vumbi , makutano na
wafungwa wengi , yalimfanya apate bakteria
ambao walimsababishia maambukizi ya Kifua
Kikuu, ” alisema Dk . Amos Zehlani katika
uchambuzi wake kuhusu uzorotaji wa
Mandela.
Dk . Zehlani ambaye huandika makala za
afya, alichambua : “Ubovu wa mapafu ya
Mandela ulisababishwa na Kifua Kikuu
ambacho alikipata gerezani .”
Daktari huyo aliongeza : “Kuna mambo mengi
husababisha maambukizi ya mapafu.
Mgandamizo wa hewa kama njia ya upitishaji
oksijeni na utoaji wa kaboni ni ndogo , kama
kuna vimelea hatari vinavyoingia na kutoka
kwenye mapafu au uingiaji wa wadudu wa
Kifua Kikuu .
“Kwa kazi ngumu alizokuwa anafanya
gerezani, lile vumbi, mtu anaumwa lakini
hapati tiba muafaka , kwanza ni mshangao
kuona amefikisha umri wa miaka 95,
amejitahidi sana, kama mwili wake
usingekuwa imara, angekufa kabla ya mwaka
1994. ”
ZUMA ALIVYOLIHUTUBIA TAIFA
Usiku wa kuamkia jana, Rais wa Afrika
Kusini, Jacob Zuma, aliutangazia ulimwengu
kupitia Televisheni ya Taifa ya Afrika Kusini
kuhusu kifo cha Mandela akisema : “Mzee
wetu amepumzika . Taifa letu limepoteza
mtoto wake bora. Watu wa taifa letu
wamempoteza baba yao. Ameondoka kwa
amani .
Akaendelea : “Mawazo yetu yanarandana na
mamilioni ya watu ambao walimkumbatia
Mandela kama mtu wao na kuona kila kitu
chake ni chao, hiki ni kipindi cha huzuni
kubwa sana.
“Tuliona ndani yake kile ambacho tunahitaji
na ndani yake tuliona mengi yenye manufaa
kwetu . Nelson Mandela alituweka pamoja ,
kwa maana hiyo tutamkumbuka .”
AFIA NYUMBANI
Mandela alifariki dunia akiwa nyumbani
kwake, Johannesburg, Afrika Kusini, baada ya
mapafu yake kushindwa kufanya kazi .
Tofauti na mara nyingine ambazo Mandela
alizidiwa na kukimbizwa hospitalini , awamu
hiyo haikuchukua muda mrefu kwa nafsi
kuacha mwili baada ya mapafu kufeli .
Kwa muda mrefu, Mandela alikuwa
akisumbuliwa na matatizo ya mfumo wa
upumuaji , maradhi ambayo inaelezwa
kwamba aliyapata kipindi akitumikia kifungo
cha miaka 27 jela .
Mara kadhaa , Mandela alizushiwa kifo, kuna
nyakati vyombo vya habari ulimwenguni
vilijazana hospitalini alipokuwa amelazwa na
kuripoti hatua kwa hatua kuhusu maendeleo
ya afya yake , huku ikiaminiwa kwamba
angekufa wakati wowote .
Siku zote anayejua siri ya kifo cha binadamu
ni Mungu pekee, maana akiwa nyumbani
akiendelea na matibabu madogomadogo,
Mandela alifariki dunia na kuacha mshtuko
na mshangao , maana imeonekana kama
‘ ameondoka kimyakimya ’ tofauti na
matarajio ya awali .
MANDELA NI SHUJAA WA DUNIA
Rais wa Marekani , Barack Obama ,
anamuelezea Mandela kama kioo kwake na
kwamba alijifunza siasa kupitia kiongozi
huyo.
“Jinsi alivyoendesha harakati dhidi ya
ubaguzi wa rangi Afrika Kusini , akakubali
kufungwa jela kwa sababu ya kutetea haki na
usawa wa wananchi wa Afrika Kusini,
ilionesha kwamba siyo mbinafsi na
alipambana kwa ajili ya wengi , hiyo
ilinihamasisha kuipenda siasa , ” Obama
aliwahi kunukuliwa .
Mandela alipewa Tuzo ya Amani ya Nobel
mwaka 1993 pia akatajwa kama mtu wa
mfano kuwahi kutokea , maana ilidhaniwa
kwamba baada ya kushinda kiti cha Urais wa
Afrika Kusini mwaka 1994 , angeweza kulipiza
kisasi kwa Makaburu ( Wazungu )
waliowanyanyasa watu weusi nyakati za
Utawala wa Ubaguzi wa Rangi nchini humo .
Kitendo cha kutolipiza kisasi , huku akiiongoza
nchi hiyo kwa miaka mitano tu kwa haki na
usawa kwa kila raia wa Afrika Kusini, ni
mambo yaliyomfanya awe na thamani kubwa
duniani.
Hata uamuzi wake wa kutotaka
kung’ ang ’ ania madaraka , umemfanya awe na
heshima kubwa leo .
ALIPOTOKA
Alizaliwa Julai 18, 1918 katika kabila la
machifu , kwenye Kijiji cha Mvezo , mjini
Transkei katika Jimbo la Eastern Cape .
Alipewa jina la Rolihlahla ambalo kwa tafsiri
ya Kabila la Xhosa maana yake ni msumbufu,
akitajwa kuwa mantiki ya jina hilo ilijionesha
namna alivyoisumbua Serikali ya Makaburu.
Akiwa na umri wa miaka nane, baba yake
alifariki na kuanzia hapo alipelekwa kulelewa
na Chifu wa Kabila la Thembu ambaye ndiye
aliyeratibu ndoa yake ya kwanza .
Mwaka 1943 , Mandela alitunukiwa Shahada
ya Sheria katika Chuo Kikuu cha Afrika Kusini
na ni nyakati hizo alijiunga na Chama cha
African National Congress ( ANC ) ambacho
alikiongoza kupigania usawa wa watu weusi
wa Afrika Kusini dhidi ya ubaguzi wa rangi na
hatimaye mwaka 1994 kuwa rais wa kwanza
mweusi, akishinda kupitia tiketi ya chama
hicho.
Mwaka 1948 , Mandela alichaguliwa kuwa
Katibu wa Jumuiya ya Vijana wa ANC ( ANC
Youth League) .
Mwaka 1962 , baada ya kuendesha harakati
nyingi za mapambano dhidi ya ubaguzi wa
rangi , alikamatwa na kufunguliwa mashtaka
ya kuhamasisha mgomo wa siku tatu, vilevile
kusafiri nje ya nchi bila kuwa na kibali .
Mwaka 1963 , nyaraka ya siri kuhusu Mandela
inayoitwa Umkotho we Sizwe ilikamatwa ,
ikidaiwa kwamba ilikuwa na vipengele 70 vya
kimapinduzi dhidi ya serikali .
MIAKA 27 JELA
Kutokana na makosa mbalimbali ambayo
baadaye yalikuja kumfanya atajwe kama
gaidi, yalisababisha afungwe jela miaka 27
kabla ya kuachiwa huru mwaka 1990 .
Alitumikia miaka 18 kwenye Gereza la Robben
Island kabla ya kuhamishiwa Pollsmoor nje
ya Jiji la Capetown .
Mwaka 1988 , alilazwa hospitalini baada ya
kugundulika ana maambukizi ya Kifua Kikuu ,
ni ugonjwa huo ambao unatajwa kuchochea
maradhi ya mapafu ambayo yamechukua
uhai wake .
Februari 11, 1990 , Mandela aliachiwa huru.
AANZA SIASA UPYA
Akiwa na umri wa miaka 71, Mandela alianza
upya harakati za siasa baada ya kutoka jela
ambazo zilimwezesha kushinda kiti cha urais
mwaka 1994 .
NDOA
Mandela alikumbana na migogoro ya ndoa ,
kwani alimtuhumu aliyekuwa mkewe, Winnie
Mandela kwamba hakuwa mwaminifu ,
akamtaliki na kumuoa mjane wa aliyekuwa
Rais wa Msumbuji , Samora Machel, Graca
ambaye aliishi naye mpaka mwisho wa uhai
wake.
Mke wake wa kwanza ni Evelyn Mase
ambaye walizaa watoto wanne kabla ya
kuachana, kisha akapata watoto wengine
wawili na Winnie. Mandela , ameacha watoto
watatu walio hai, kwani wengine watatu
( wote mama ni yao ni Evelyn) , walifariki dunia
kabla ya baba yao.
Saturday, December 7, 2013
UNDANI KIFO CHA MANDELA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment