Tuesday, December 10, 2013

LINAH : NASAKA MIMBA


STAA wa Bongo Fleva , Estelina Sanga ‘ Linah’
juzikati ameweka wazi nia yake ya kusaka
mtoto , Risasi Mchanganyiko linakushushia .
Estelina Sanga ‘Linah ’ .
Akizungumza na mwandishi wetu Desemba
9, mwaka huu jijini Dar , Linah alisema tangu
alipoingia kwenye muziki hakuwahi kufikiria
kushika ujauzito kwa kuwa alikuwa bado
hajajiandaa kufanya hivyo .
Nyota huyo ambaye aliwahi kuzama katika
penzi zito la staa mwenzake , Amin
Mwinyimkuu alisema kuwa kwa sasa hali ni
tofauti na anataka kuzaa iwapo atashika
ujauzito .
“Nilipokuwa katika uhusiano wangu wa
kwanza hakuna hata siku moja niliyohisi
kama nitakuja kutamani kupata mtoto maana
mwenzangu aliponiambia tuzae nilimkatalia
tofauti na leo hii natamani nishike mimba na
ulimwengu wote ujue kwamba nina mimba , ”
alisema Linah .
Hata hivyo Linah alikwepa kuweka wazi
uhusiano wake wa sasa na hakutaka
kumwongelea Amin .

1 comment:

.