Kocha Mkuu wa Simba , Zdravok Logarusic.
Na Khatimu Naheka
KOCHA Mkuu wa Simba, Zdravok Logarusic
amelazimika kubadili ratiba ya mazoezi ya
kikosi chake , kikubwa ni kuifuata Yanga
itakayovaana na KMKM kesho Jumamosi .
Akizungumza na Championi Ijumaa,
Logarusic , raia wa Croatia , amesema
atakuwepo kwenye Uwanja wa Taifa jijini
Dar , kuiangalia Yanga itakapokuwa ikiumana
na KMKM ya Zanzibar katika mchezo huo wa
kirafiki ambapo atafika hapo akiwa na peni
na karatasi ndogo .
Logarusic ‘ Loga ’ amesema hajawahi
kuishuhudia ‘ live’ Yanga ikicheza, ambapo
sasa atautumia mchezo huo kama njia ya
kukisoma kikosi hicho kilicho chini ya Ernie
Brandts raia wa Uholanzi lakini uamuzi huo
utamfanya avunje ratiba ya mazoezi ya jioni
ya timu yake.
“Nimesikia kuwa Yanga wanacheza
Jumamosi na ile timu tutakayocheza nayo
sisi Jumapili , nadhani nitabadili ratiba ya
mazoezi kwa kufanya asubuhi ili niweze
kwenda kuiona hiyo mechi , nataka kuwaona
jinsi walivyo na nitafika na kalamu moja na
kipande cha karatasi pekee, ” alisema Loga .
Wakati huohuo waandaaji wa mchezo huo ,
Kampuni ya Smart Sports , wametaja viingilio
vya mechi hizo mbili za kirafiki kuwa , VIP A
ni shilingi 20 , 000, VIP B Sh 15, 000 , VIP C Sh
10, 000 wakati viti vya rangi ya machungwa
Sh 7, 000 huku vile vya bluu na kijani ikiwa Sh
5, 000.
hope
Friday, December 13, 2013
Logarusic avunja mazoezi Simba , aifuata Yanga Taifa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment