Friday, December 13, 2013

Minziro : Julio fanya kazi, punguza kelele


Na Martha Mboma na Lucy Mgina
KOCHA Msaidizi wa Yanga, Felix Minziro
amemwambia aliyekuwa Kocha Msaidizi wa
Simba, Jamhuri Kihwelo ‘ Julio’ apunguze
kuzungumza, badala yake afanye kazi .
Julio hivi karibuni alitimuliwa na Simba
pamoja na aliyekuwa Kocha Mkuu, Abdallah
Kibadeni ambaye sasa ametua Ashanti
United.
Minziro amesema Julio ana uwezo mkubwa
wa kufundisha , kikubwa kinachomponza ni
kelele anazozipiga kitu ambacho siyo sahihi .
“Nampa ushauri wa bure mdogo wangu Julio,
ili adumu kwenye timu zetu za Bongo muda
mrefu, basi aache kelele , badala yake afanye
kazi pekee, ninaamini atafanikiwa zaidi ya
hapo alipo.
“Julio ana uwezo mkubwa wa kufundisha
soka , anaingia kwenye orodha ya makocha
bora nchini kutokana na uwezo wake
mkubwa, kama akiufanyia kazi ushauri
wangu, atafika mbali, ” alisema Minziro .

No comments:

Post a Comment

.