Friday, December 13, 2013

Matuta yaizamisha Kili Stars


Na Mwandishi Wetu
TIMU ya taifa ya Tanzania Bara, Kilimanjaro
Stars imeikosa nafasi ya tatu katika
Michuano ya Chalenji iliyomalizika jana
nchini Kenya , baada ya kufungwa na Zambia
kwa mikwaju ya penalti 6 -5.
Katika mchezo huo uliopigwa majira ya saa
8: 00 mchana kwenye Uwanja wa Nyayo jijini
Nairobi, dakika 90 zilimalizika kwa timu hizo
kufungana bao 1 -1, ambapo penalti
iliyopigwa na nahodha wa Stars , Kelvin
Yondani iliota mbawa na kuipa ushindi
Zambia.
Zambia ndiyo walikuwa wa kwanza kupata
bao katika dakika ya 52 kupitia kwa kiungo
mshambuliaji , Ronald Kampamba .
Katika dakika ya 60 , Kocha Mkuu wa Stars ,
Kim Poulsen alifanya mabadiliko kwa
kuwatoa Hassani Dilunga na Athumani Idd
‘ Chuji ’ na kuwaingiza Ramadhani Singano
‘ Messi ’ na Haruna Chanongo .
Kuingia kwa wachezaji hao kulibadilisha
mchezo wa Stars ambao walianza
kulishambulia goli la wapinzani wao na
dakika 64 mshambuliaji wa kimataifa wa TP
Mazembe ya DR Congo, Mbwana Samatta ,
akaisawazishia Stars .
Waliofunga penalti za Stars ni Samatta ,
Erasto Nyoni, Himid Mao , Amri Kiemba na
Singano huku waliokosa ni Chanongo , Mrisho
Ngassa na Yondani.
Mpaka gazeti hili linaelekea mitamboni ,
mechi ya fainali ilikuwa ikiendelea kati ya
Kenya dhidi ya Sudan.

No comments:

Post a Comment

.