Tuesday, December 10, 2013

MAAJABU 10 MSIBA WA MANDELA


Stori: Na Waandishi Wetu
RAIS wa zamani wa Afrika Kusini, Mzee
Nelson Mandela , mweusi wa kwanza kushika
wadhifa huo katika taifa lenye uwezo mkubwa
kiuchumi na kijeshi barani Afrika, alifariki
dunia Alhamisi iliyopita akiwa nyumbani
kwake jijini Johannesburg .
Nelson Mandela .
Kifo chake kimeushtua ulimwengu na kwa
mara ya kwanza katika historia, dunia nzima
imesimama nyuma ya jemedari huyo, kila
mmoja akionesha masikitiko yake.
Wakati dunia ikisubiri mazishi yake ambayo
pia yatavunja rekodi ya mazishi yote
yaliyowahi kufanywa tokea kuumbwa kwa
uso wa dunia hapo Desemba 15 mwaka huu,
Uwazi limebaini maajabu kumi
yanayoambatana na msiba huo.
AIR FORCE ONE KUBEBA MARAIS WATANO
WA MAREKANI
AIR Force One ni ndege inayombeba Rais wa
Marekani aliye madarakani na kumpeleka
popote duniani . Lakini katika hali ya
kushangaza, Idara ya Usalama ya Marekani
imetoa ruhusa kwa marais wastaafu wakiwa
na wake zao, kuandamana na Rais Barak
Obama kuhudhuria mazishi ya shujaa huyo
wa dunia .
Hii ni mara ya kwanza katika historia ya taifa
hilo lenye nguvu kubwa duniani kuwapakia
katika ndege hiyo yenye kila kitu ndani yake ,
marais wake kwa wakati mmoja .
Marais hao ni Obama mwenyewe na mkewe
Michelle, George Bush na mkewe Laura, Bill
Clinton na mkewe Hillary, Rais wa 39 wa
Marekani , Jimmy Carter naye atakuwepo ila
baba yake George W. Bush , George Bush
senior huenda asiende kutokana na urefu wa
safari hiyo .
QUNU; KIJIJI KITAKACHOLNDWA KULIKO
VYOTE DUNIANI
Mandela alizaliwa katika Kijiji cha Qunu ,
kilichopo katika Jimbo la Eastern Cape ,
kilometa 32 Kusini Magharibi mwa mji wa
Mthatha.
Kutokana na tukio hilo kubwa la mazishi ,
Jeshi la Afrika Kusini ambalo ni bora zaidi
barani Afrika, limechukua jukumu la
kusimamia ulinzi wote. Lakini uwepo wa Rais
Obama na watangulizi wake wanne , utaifanya
nchi hiyo kuchukua tahadhari zaidi ya
kuhakikisha hakuna dosari yoyote ya
kiusalama inayoweza kujitokeza .
Ulinzi huo umeimarishwa zaidi kutokana na
ukweli kwamba viongozi wakubwa karibu
wote wa dunia watahudhuria mazishi hayo,
akiwemo Papa Francisco, Waziri Mkuu wa
Uingereza, David Cameron na Katibu Mkuu
wa Umoja wa Mataifa , Ban Ki Moon . Hakuna
uwezekano wowote wa Al shaabab
kusababisha rabsha kwani wameshadhibitiwa
kwa ulinzi mkali.
MANDELA ALIKUWA ‘GAIDI’ PEKEE
ALIYEGEUKA KUWA SHUJAA
Kwa miaka mingi , mataifa ya magharibi
pamoja na Marekani walimchukulia Mandela
na harakati zake kama gaidi . Wakati wa
utawala wa ubaguzi wa rangi nchini Afrika
Kusini, chama cha ANC kilikuwa na jeshi lake
lililofahamika kama Umkhonto we Sizwe .
Wazungu wa Magharibi na Marekani ambao
walikuwa wakiwaunga mkono Makaburu,
waliiona ANC kama kikundi cha kigaidi na
hivyo Mandela naye akawekwa katika orodha
ya magaidi duniani.
Hata hivyo , baada ya kutoka jela na
kuchaguliwa kuwa Rais wa Afrika Kusini,
Mandela aligeuka kuwa kipenzi cha watu hao
ambao walilazimika kumuondoa katika
orodha ya magaidi na leo hii akiwa amefariki
dunia, anapewa heshima kubwa kuliko
aliyowahi kupewa mzungu yeyote duniani .
MWEUSI PEKEE ALIYENYENYEKEWA NA
WAZUNGU
Hayati Mandela ndiye mtu mweusi pekee
duniani aliyewahi kupewa heshima zisizo na
mfano tokea kuumbwa kwa dunia . Mara
baada ya kutangazwa kwa kifo chake,
viongozi wa mataifa yote makubwa duniani
walionesha masikitiko yao na kila mmoja
alimsifu kama mtu wa aina ya pekee kuwahi
kuwepo chini ya jua ( ukiachia mbali mitume
na manabii ) .
JENGO LA SERIKALI NEW YORK LAPAKWA
RANGI YA BENDERA YA SAUZI
Jengo moja la serikali jijini New York,
Marekani limebadilishwa taa za kulipamba na
kuonesha bendera ya taifa la Afrika Kusini.
WENYEJI WAHAMA , WAGENI WAMILIKI
NYUMBA QUNU
Kijiji cha Qunu , sehemu ambayo yatafanyika
mazishi ya Mandela , kuna eneo dogo
kulingana na ugeni mkubwa unaotarajiwa
kuwepo. Taarifa kutoka huko zinasema
wenyeji , pamoja na machungu waliyonayo
kutokana na kifo cha mzee huyo, pia
watafaidika kiuchumi kutokana na wageni
wengi kutaka kupata nyumba za kukaa
wakati wakiendelea na maombolezo .
Wanaotafuta nyumba kijijini hapo ni pamoja
na watu kutoka vyombo mbalimbali vya
habari, mashirika ya kimataifa na wageni
binafsi.
Inadaiwa kuwa wenyeji wanasogea katika
vijiji vya jirani ili kupangisha nyumba zao kwa
muda .
MECHI ZA LIGI KUU ENGLAND ZAANZA KWA
SALA
Katika hali isiyokuwa ya kawaida , Chama cha
Soka cha England ( FA ) kiliamuru mechi zote
za ligi kuu zilizochezwa wiki iliyopita, lazima
zianze kwa sala maalum ya kumuenzi mzee
Mandela.
Hii ni mara ya kwanza kwa agizo hilo
kutolewa kwa heshima ya kiongozi mstaafu
aliyefariki dunia asiye Mwingereza, tena
akitokea barani Afrika. Tukio kama hilo pia
limefanywa na Shirikisho la Soka la Kimataifa
( FIFA) ambalo limeamuru bendera yake iliyo
katika mataifa yote wanachama duniani,
ishushwe nusu mlingoti kwa heshima ya Tata
Madiba !
NASA YATOA ZAWADI YA PICHA YA SAUZI
KUTOKA ANGANI
Taasisi ya utafiti wa anga za juu nchini
Marekani ( NASA ) kwa kutambua mchango
mkubwa wa Mandela katika amani ya dunia ,
imetangaza kutoa zawadi kwa watu wa
Afrika Kusini , itakayoonesha picha ya nchi
hiyo inavyoonekana kutoka angani .
UINGEREZA YAAGIZA BALOZI ZOTE
KUSHUSHA NUSU MLINGOTI
Serikali ya Uingereza imeziagiza balozi zote
za kigeni zilizopo nchini humo kushusha
bendera zao nusu mlingoti kama moja ya
heshima na maombolezo ya kifo cha Mzee
Nelson Mandela .
Hili ni agizo la aina yake kuwahi kutolewa
kuhusiana na msiba wa kiongozi yeyote ,
kwani suala la kushusha bendera mara nyingi
ni uamuzi wa serikali husika na si kwa
shinikizo kama ilivyotokea Uingereza.
AMSAFIRISHA PAPA MAZISHINI
Historia ya utumishi wa kiongozi mkuu wa
Madhehebu ya Romani , papa haioneshi kama
aliwahi kuhudhuria mazishi ya rais au rais
mstaafu, kitendo cha Papa Francisco
kuhudhuria mazishi hayo kumeongeza ajabu
katika mazishi ya Mandela , wengi wakisema
hakina hakuwa mtu wa kawaida .

No comments:

Post a Comment

.