Stori: Haruni Sanchawa na Imelda Mtema
KIFO cha ghafla cha mtoto Suleiman Rajabu
( 17) aliyekuwa na tatizo la mguu mmoja
kuvimba tangu utoto kilichotokea Desemba 6 ,
2013 nyumbani kwao , Kitunda - Kivule
‘ Bombambili ’ , Dar kimeibua mengi, lakini zito
ni ushirikina kuhusishwa, Uwazi limeambiwa .
Suleiman ilikuwa apelekwe India kwa
matibabu, Desemba 8, 2013. Maandalizi yote
ya safari yalishakamilika .
Baadhi ya ndugu waliozungumza na Uwazi
msibani hapo , walitoa sauti zao wakituhumu
kuwa kuna mkono wa mtu katika kifo hicho
kutokana na mazingira yake .
Ndugu mmoja ndani ya wanafamilia ambaye
hakutaka jina lake liandikwe gazetini alisema
kilichomsukuma kunena hayo kwa ujasiri ni
kuona kwamba mtoto huyo alizaliwa na
tatizo hilo, sasa ana miaka 17 na katika
muda wote familia ilihangaika kutafuta tiba ,
“iweje leo , siku moja kabla ya kusafirishwa
kwenda India kwa matibabu ndiyo afariki
dunia?
“Kufa kupo lakini kwa Suleiman aliyeishi kwa
mateso kwa miaka kumi na saba mpaka
juzijuzi tu Kampuni ya Global Publishers
ikaandika habari zake na watu wakamsaidia
mtoto , iweje afe siku moja tu kabla ya
safari ?” alihoji ndugu huyo.
Waombolezaji wengi waliokutwa msibani
hapo pia nao walizungumzia uwezekano wa
ushirikina kuhusishwa .”
Habari za ugonjwa wa mtoto huyo zilikuwa
zikiandikwa na Magazeti Pendwa ya Global
Publishers ambapo picha yake pia ilionesha
jinsi mguu mmoja ulivyovimba kimaajabu na
kumfanya ashindwe kutembea maishani
mwake .
Familia yake iliomba msaada kwa wasamaria
wema ili mtoto huyo atibiwe. Awali baada ya
kupata kiasi cha fedha, alipelekwa Hospitali
ya CCBRT ya jijini Dar ambako walishauri
apelekwe India .
Mmoja wa watu walioguswa na kumlilia
mtoto huyo kabla na baada ya kifo ni
mtangazaji wa televisheni wa kituo cha
Channel Ten ambaye pia ni Miss Tanzania
1999, Hoyce Temu ambaye pamoja na
masikitiko yake alianzisha utaratibu wa
kutafuta njia za kumsaidia mgonjwa huyo
kupitia kipindi chake cha Mimi na Tanzania
kinachorushwa hewani na Runinga hiyo na
kutoa misaada mbalimbali ya hali na mali.
Kupitia kipindi hicho na magazeti ya Global,
michango iliyokusanywa ili kumsaidia ilifikia
shilingi milioni 13 ambapo sehemu ya fedha
hizo zilishalipwa kwenye Hospitali ya Ganga,
India ambako marehemu ilikuwa apelekwe
kwa matibabu Jumapili iliyopita .
Mratibu wa safari iliyokufa ya Suleiman ,
Imelda Mtema ambaye ni mwandishi wa
habari wa Global Publishers alisema juzi
kuwa , kwa vile fedha za kumlipia marehemu
zilishalipwa India na haziwezi kurudishwa,
mtoto Hamis Hashim ambaye naye ana
tatizo kama la marehemu Suleiman
atapelekwa nchini humo kutibiwa.
Baba mzazi wa Suleiman , Rajabu Upinde
aliwashukuru wote walioguswa na mwanaye
hasa walioendesha harakati za kufanikisha
michango ya mtoto huyo lakini akasema
haikuwa riziki .
Mazishi ya Suleiman Rajabu yalifanyika
Desemba 7, mwaka huu Mwaneromango ,
wilayani Kisarawe mkoani Pwani. Mungu
ailaze pema peponi roho ya marehemu.
Amina.
Tuesday, December 10, 2013
USHIRIKIANA WATAJWA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment