BAADA ya kudaiwa kufanya ngono katika
magari ya Kampuni ya Endless Fame
inayoongozwa na Wema Issac Sepetu ,
Prodyuza, Rashid Mohammed ‘ Chid Classic’
amefunguka na kusema chanzo cha yote ni
mshahara na ukuwadi ndani ya kampuni
hiyo wala siyo uzinzi , Amani linakujuza .
Prodyuza Rashid Mohammed ‘ Chid Classic ’.
Akizungumza na mwandishi wa gazeti hili ,
Chid amesema hajafukuzwa katika kampuni
hiyo kama alivyodai mratibu wa kampuni
hiyo , Petit Man bali ameondoka baada ya
kuchoka kufanya kazi bila ya kulipwa
mshahara.
“Ni uongo kusema kwamba nimenaswa
nikifanya uzinzi Coco Beach nikiwa ndani ya
magari ya Wema , sijawahi hata siku moja
kufanya hivyo kwani nina kwangu ambako
nina uwezo wa kumwingiza mwanamke
wakati wowote ,” alisema .
Wema Isaac Sepetu .
“Tangu kampuni ianzishwe haijawahi kulipa
mishahara unadhani nitakuwa na moyo wa
kufanya kazi , sikwenda pale kufanya ukuwadi
kama wengine, tena nawaomba wasiendelee
kusema uongo kwani nina mengi nayajua ya
Endless Fame, ” aliongeza Chid.
Baada ya kusikia maelezo hayo, Amani
lilimtafuta Wema bila ya mafanikio ndipo
likaongea na meneja wake, Martin Kadinda.
“Nina wasiwasi na kauli za Chid kwanza
tatizo siyo mshahara na hayo masuala ya
ukuwadi ni uongo na uzushi , kama ni kweli
kwa nini asiongee siku zote hadi lilipoibuka
hili la kunaswa akifanya uzinzi kwenye gari ?”
alihoji Kadinda.
Thursday, December 12, 2013
PRODYUZA: WEMA ALITAKA NIWE KUWADI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Team Wema
ReplyDelete