Rais mstaafu wa Afrika Kusini, Nelson
Mandela .
HABARI kutoka Johannesburg, zinasema rais
mstaafu wa Afrika Kusini, Nelson Mandela ,
anaendelea kupigana dhidi ya kifo kutoka
kitandani ambako wanafamilia wake
wamelieleza Shirika la Utangazaji la Afrika
Kusini ( SABC ) kwamba : “Baba bado yuko
nasi , akiwa shupavu kutoka katika kitanda
chake cha kifo ambako anaendelea
kutufundisha kuhusu kuwa na subira , upendo
na uvumilivu .”
Hayo yalisemwa na binti yake , Makaziwe
Mandela, aliyeongeza kwamba anaona fahari
kuwa sehemu ya mtu huyo ambaye bado ni
mpiganaji japokuwa anafanya hivyo kwa
shida.
Mandela alikaa karibu miezi mitatu katika
hospitali moja jijini Pretoria kutokana na
kusakamwa na ugonjwa wa mapafu kila
mara. Shujaa huyo wa vita vya ukombozi
mwenye umri wa miaka 95 aliondoka
hospitalini mwezi Septemba na anapata
matibabu nyumbani tangu wakati huo .
Tangu wakati huo, serikali imekuwa ikisema
hali yake ni mbaya lakini yenye matumaini ,
ambapo mjukuu wake, Ndaba Mandela ,
aliliambia SABC kwamba : “Bado yuko nasi
japokuwa hali yake kitandani si nzuri .”
Wednesday, December 4, 2013
MANDELA AENDELEA KUPIGANA DHIDI YA KIFO KUTOKA KITANDANI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment