Lawrence Mwalusako akiongea na waandishi
wa habari ( picha na maktaba )
Uongozi wa klabu ya Young Africans leo
umetoa ripoti ya mapato na matumizi kwa
kipindi cha miezi sita tangu Januari 14 , 2013
mpaka Julai 14 , 2013 ikiwa ni sehemu ya
muendelezo wa kutoa mahesabu hayo kwa
wapenzi, washabiki , na wanachama na jamii
kwa ujumla .
Baadhi ya gharama kubwa kwa klabu ni
pamoja na usajili wachezaji na
mishahara.Akiongea na waandishi wa habari
juu ya mahesabu hayo katibu mkuu wa
Young Africans Lawrence Mwalusako
amesema mapato makubwa ya klabu
yanatokana na viingilio vya mechi na ufadhili .
Juhudi mbalilmbali zinafanyika
kuongeza kipato cha klabu kama
kuingia mikataba ya ufadhili , kutumia
haki miliki za klabu.
Uongozi unajitahid kuweza kudhibiti
matumizi ya klabu kama njia moja ya
kuhakikisha klabu inajitegemea.
Klabu bado inaendelea kutegemea
ufadhili wa TBL ambao kwa sasa
inapata wastani wa mIL 30. 25 kila
mwezi , Madhumuni ya ufadhili huu ni
kuwezesha klabu kulipia mishahara
ambayo wastani inzaidi mil 60 kwa
mwezi . Tayari klabu imeshaomba
mazungumzo na mfadhili kuboresha
mkataba huo .
Katika kipindi cha Januari 2013 hadi
Julai 2013 klabu iliweza kupata mil
110 kama zwadi mbalii mbali za
ushindi ikiwemo mil 15 kutoka
vodacom kwa kuwa timu yenye
nidhamu .
Bado kuna mali za klabu hazija
thaminiwa zikiwemo majengo.
CHANZO NI TOVUTI YA YANGA FC
Wednesday, December 4, 2013
YANGA YATOA RIPOTI YA MAPATO NA MATUMIZI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment