Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Yusuf Manji .
Na Hans Mloli
MWENYEKITI wa Klabu ya Yanga, Yusuf
Manji, ametangaza rasmi kutowania tena
nafasi ya uenyekiti kwenye uchaguzi mkuu
wa klabu hiyo utakaotangazwa baadaye
mwakani.
Manji alichukua wadhifa huo mwaka jana
baada ya kuondolewa kwa aliyekuwa
Mwenyekiti, Lloyd Nchunga , aliyekuwa
amebakiza miaka miwili ya uongozi wake
klabuni hapo .
Manji ambaye pia ni mfadhili wa klabu hiyo
alitoa tamko juu ya nia yake hiyo jana
kwenye makao makuu ya klabu hiyo yaliyopo
Jangwani, Kariakoo jijini Dar es Salaam huku
akitoa sababu kuwa ni kuwapisha wengine
wenye uwezo wa kuiongoza timu hiyo nao
kuchukua jahazi .
Amesema ametangaza kutowania nafasi hiyo
mapema ili kuwapa nafasi nzuri wanaotaka
kufanya hivyo wajipange mapema .
“Sitagombea tena uenyekiti kwenye uchaguzi
ujao, nitawaachia wengine waendeleze hapa
nilipoishia mimi , nimetangaza mapema ili
wanaoitaka hii nafasi wajipange , maana
wapo wenye nia lakini wanahofia kuchuana
na mimi .
“Ninaweza kugombea lakini si sasa labda
baadaye na siyo uchaguzi huu, nitafikiria
kwanza kabla ya maamuzi hayo, ” alisema
Manji.
Kiongozi huyo aliongeza kuwa ataendelea
kuiongoza Yanga kwa miezi saba iliyosalia.
Aidha , alisema kuwa bado tarehe rasmi ya
uchaguzi huo haijafahamika na kudai kuwa
itajulikana mara baada ya Mkutano Mkuu wa
Yanga utakaofanyika Januari 19 , mwakani.
“Nikishajitoa rasmi kwenye madaraka ya
uongozi wa Yanga baada ya kuwa
nimemaliza muda wangu nitaendelea kuwa
shabiki wa kawaida wa Yanga kama ilivyo
kwa wengine na kuhusu udhamini litabaki
kuwa suala la klabu kuchagua mdhamini
wao , ” alisema Manji .
Thursday, December 12, 2013
Manji ajitoa Yanga SC
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment