Wanajeshi wakiwa wameubeba mwili wa
hayati Mandela kuelekea ofisi za serikali
jijini Pretoria.
Mwandishi Wetu na Mitandao
MAOMBOLEZO ya kifo cha aliyekuwa rais wa
kwanza mweusi nchini Afrika Kusini , Nelson
Mandela yanaendelea , kubwa kuliko ni nchi
hiyo yenye kilomita za mraba 2, 798 kufurika
waombolezaji kutoka pande zote za dunia na
hivyo , hakuna pa kukanyaga na hali hii ni
mwanzo na mwisho !
Nelson Mandela .
Habari kutoka jijini Johannesburg nchini
humo zinasema , msiba wa Mandela
umebadilisha ghafla hali ya maisha ya raia
wa nchi hiyo .
HOTELI HAZINA NAFASI
Hoteli nyingi , hasa katika Miji ya Pretoria na
Johannesburg ( alikofia Mandela ) , nyumba za
kulala wageni , hoteli na sehemu nyingine
zenye kuhifadhi watu zimejaa baada ya
wateja kukodi kwa muda wote wa msiba hadi
mazishi .
Wageni wanaoingia nchini humo kwa ratiba
zao za kabla ya kifo wamekuwa wakipata
tabu sehemu za kulala , wengine kugeuza
wanakotoka.
Familia ya marehemu Mandela ikifuatilia
ibada ya kumbukumbu .
Baadhi ya wenyeji waishio nchini humo
wamewasiliana na ndugu zao wanaotaka
kwenda, kusitisha safari ili kupisha shughuli
za mazishi yatakayofanyika Desemba 15,
mwaka huu .
BIDHAA BEI JUU
Licha ya kwamba kipato cha kawaida kwa
wananchi wake ni cha chini , bei ya bidhaa ,
hasa vyakula imepanda na wafanyabiashara
wengi wanaitumia fursa hiyo kujineemesha.
Rais wa Marekani, Barrack Obama
akiwapungia maelfu ya wananchi
waliohudhuria ibada ya kumkumbuka
Mandela katika Uwanja wa FNB , Soweto ,
Afrika Kusini.
MIPAKA HAIPITIKI KAMA ZAMANI
Tofauti na hali ilivyokuwa kabla ya kifo cha
Mandela ambapo wengi waliweza kuingia
nchini humo bila kubanwa na ukaguzi wa
kina , kwa sasa ulinzi umeimarishwa ambapo
kila muingiaji anaulizwa maswali mengi , hasa
yanayohusu usalama .
MAGAIDI WATUPIWA MACHO ZAIDI
Usalama nchini humo tangu kutokea kwa kifo
cha Mandela umekuwa ukiwatupia macho
zaidi magaidi wa kimataifa ambao wanaweza
kutumia mwanya wa maombolezo kupenya
na kusababisha maafa.
Baadhi ya waombolezaji.
GRACA MACHEL , WINNIE MANDELA
HAKUNA BIFU
Juzi ndani ya Uwanja wa FNB uliopo Mtaa
wa Soccer City nchini humo wakati wa zoezi
la kumuaga marehemu Mandela , kivutio
kikubwa kilikuwa kwa wanawake wawili
waliowahi kuwa na uhusiano na kiongozi
huyo.
Winnie Medekizela Mandela , aliyewahi kuwa
mke wa Mandela mpaka kutoka kifungoni na
Graca Machel aliyekuwa mke mpaka kifo cha
Mandela, walitazamwa na waombolezaji
wengi kufuatia historia zao kutokuwa na
migongano.
Wawili hao , mara kadhaa wamewahi kupiga
picha ya pamoja na mzee huyo wakiwa na
nyuso za furaha huku wote wakiwa
wamemkumbatia.
Viongozi mbalimbali akiwemo Rais Jakaya
Kikwete ( wa nne mstari wa pili kulia kutoka
juu ) na mkewe Mama Salma wakifuatilia
ibada ya kumbukumbu ya Nelson Mandela .
OBAMA AHUTUBIA NDANI YA JUKWAA
LENYE VIOO VYA KUKINGA RISASI
Akitoa hotuba yake kwa wananchi wa Sauzi
na waombolezaji wengine duniani kote, Rais
wa Marekani , Barack Obama alionekana
ndani ya jukwaa lenye vioo visivyoweza
kupitwa na risasi ( bullet proof) .
DUNIA YAANDIKA HISTORIA MPYA
Kuwepo kwa Rais wa Marekani , Barack
Obama na Rais wa China, Xi -Jinping
kunasemekana ni kuandikwa kwa historia
mpya ya dunia kwani viongozi hao
hawajawahi kukutana nje ya nchi zao.
Kingine kilichoonekana ni kuandikwa kwa
historia mpya ya dunia ni tukio hilo kuwa la
kwanza kukutanisha viongozi wazito wa
duniani kwa wakati mmoja .
Inadaiwa hata wanaokwenda kwenye
mkutano wa Umoja wa Mataifa hawakufikia
uzito wa kwenye msiba wa Mandela .
Marais mbalimbali wakiambatana na ujumbe
mzito kutoka katika nchi zao walihudhuria
msiba huo , ukiachana na watu wengine
maarufu na viongozi wa kawaida .
JINA LA KIKWETE LAWA LA KWANZA
KWENYE ORODHA
Katika hali iliyoonesha mshikamano kati ya
Afrika Kusini na Tanzania , jina la Rais Jakaya
Kikwete lilikuwa la kwanza katika orodha ya
marais waliokuwa kwenye mwaliko .
Jambo hilo limeongeza hamasa na uhusika
wa moja kwa moja kwa Watanzania juu ya
msiba huo kutokana na umoja , ushirikiano na
kuaminiana kulikooneshwa na Sauzi .
Juzi , Jumatatu , Desemba 9 , mwaka huu
katika sherehe za Miaka 52 ya Uhuru ,
zilizofanyika kitaifa , Uwanja wa Uhuru , Dar ,
Rais Kikwete alizungumzia namna marehemu
Mandela alivyoipenda Tanzania na uhusiano
mwema wa nchi hizi mbili.
Hilo lilijidhihirisha baada ya Sauzi kumweka
Rais Kikwete wa kwanza , akiwaongoza
marais na viongozi wengine waliohudhuria
msiba na shughuli za mazishi ya shujaa
huyo.
NAMBA 3 YAWAMALIZA VIGOGO NCHINI
HUMO
Pamoja na yote, namba 3 imeonekana
kuweka historia ya kipekee nchini humo kwa
kuhusika na vifo vya viongozi wake wakuu .
Mpigania haki mwingine mkongwe , Oliver
Tambo aliyezaliwa Oktoba 27 , 1917 naye
alifariki mwaka 1993 ( Aprili 24) . Walter
Sisulu, alikuwa mpigania uhuru sambamba na
Tambo na Mandela , naye alifariki dunia
mwaka 2003 ( Mei 5, alizaliwa Mei 18 , 1912 ) .
Kifo cha Mandela kilichotokea Desemba 5,
2013 kinazidi kutia shaka katika orodha ya
namba 3 kila baada ya miaka 10 .
Marehemu Nelson Mandela ambaye zoezi la
kuuaga mwili wake linakamilika leo kwenye
uwanja huo , atazikwa Jumapili ijayo . Mungu
ailaze roho yake mahala pema peponi -
Amina.
Thursday, December 12, 2013
SAUZI YAJAA MSIBA WA MANDELA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment