Akimnyooshea kidole, acha mambo yako
mwana!: Per Mertesacker (kulia)
akimuwakia Mesut Ozil baada ya kula
kipigo cha mabao 6-3 kutoka kwa
Manchester City
KIPIGO siku zote kinavuruga!!. Baada ya
Arsenal kuburuzwa kwa kipigo cha mabao
6-3 kutoka kwa Manchester City, Wachezaji
wawili wa klabu hiyo raia wa
Ujerumani, Per Mertesacker na Mesut Ozil
wamepigana mkwara mzito wakati
wakitoka nje ya uwanja wa Etihad.
Mertesacker alimuwakia vikali Ozil ambaye
ni rafiki mkubwa katika soka na
kumnyooshea kidole kiungo huyo baada ya
kipenga cha mwisho kupulizwa.
Hali hiyo imetokea baada ta Ozil kushindwa
kuwapungia mkono wa heshima mashabiki
wa Gunners waliosafiri ugenini.
Wakati wawili hao wakizozana, kocha
mkuu wa klabu hiyo, Arsene Wenger
alicheka tu na kusema: “Waache
Wajurumani, watamalizana wenyewe,
msijali”.
Mabao ya City yamefungwa na Sergio
Aguero dakika ya 14, Alvaro Negredo dakika
ya 39 Fernandinho mawili dakika za 50 na
88 David Silva dakika ya 66 na Yaya Toure
dakika ya 90.
Theo Walcott alirejea uwanjani kwa mara
ya kwanza leo tangu Septemba na
kufanikiwa kutundika nyavuni mabao
mawili ya Arsenal dakika za 31 na 63,
wakati lingine lilifungwa na beki Per
Mertesacker dakika ya 90.
Acha hizo!: Mertesacker akiendelea
kumuwakia rafiki yake mkubwa katika
soka
Wakionesha mfano: Jack Wilshere (kushoto)
na Mertesacker wakionesha heshima kwa
mashabiki waliosafiri leo
Katika mechi nyingine leo, Fernando Torres
alifunga bao mojawapo katika ushindi wa
mabao 2-1 dhidi ya Crystal Palace na
kuifanya Chelsea iwe nyuma kwa pointi
mbili na vinara Asernal ambao leo
wamekula kisago kikubwa kutoka kwa Man
City.
Bao lingine la Chelsea limefungwa na
Mbrazil, Ramirez katika dakika ya 35
akipokea pasi kutoka kwa Eden Hazard.
Bao la kufutia machozi kwa Crystal Palace
limefungwa na mashambuliaji wake raia wa
Morocco, Marouane Chamakh.
Kocha Jose Mourinho anaamini kuwa
haiwezekani hata kidogo kuwafananisha
washambuliaji wake na vijana wenye kipaji
kikubwa na maarifa ya soka wa klabu ya
Man City, Sergio Kun Aguero au Luis Suarez
wa Liverpool.
Kupingana na mtazamo wa kocha wake,
Torres alifunga bao la kwanza ambalo
linamaanisha Chelsea watakwea kileleni
kabla ya krimasi endapo wataifunga
Arsenal katika dimba la Emirates desemba
23 mwaka huu.
Ramires aliifungia Chelsea bao la pili
Kikosi cha Chelsea: Cech 5; Ivanovic 6, Luiz
6, Terry 6, Azpilicuta 7; Essien 6, Ramires 7;
Willian 7 (Schurrle 82), Mata 5 (Oscar 62, 5),
Hazard 6; Torres 5 (Ba 84).
Crystal Palace: Speroni 8; Mariappa 6,
Gabbidon 7, Delaney 6, Ward 7; Bannan 5
(Bolasie 51, 5), Jedinak 7, Dikgacoi 5
(O’Keefe 26, 7), Puncheon 6; Chamakh 7
(Gayle 88), Jerome 7.
Shock on the cards: Marouane Chamakh
continues his good form infront of goal by
making it 1-1
Amerudi mchezoni: Chamakh akirudisha
matumaini kwa Palace baada ya
kusawazisha na kufanya ubao usomeke 1-1
Mourinho naweza baba!: Fernando Torres
akishangilia bao la kwanza dhidi ya Palace
Mechi zilizomalizika matokeo yako
ifuatavyo;
England: Premier League
Finished Manchester City 6-3 Arsenal (2-1)
Finished West Ham 0-0 Sunderland (0-0)
Finished Newcastle United 1-1 Southampton (1-0)
Finished Everton 4-1 Fulham (1-0)
Finished Chelsea 2-1 Crystal Palace (2-1)
Finished Cardiff 1-0 West Bromwich Albion
Sunday, December 15, 2013
MERTESACKER, OZIL NUSURA WAZICHAPE KUFUATIA KIPIGO CHA 6-3,
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment